IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /27

Hatari za haraka yenye muelekeo hasi

15:41 - September 18, 2023
Habari ID: 3477618
TEHRAN (IQNA) – Watu wanahitaji utulivu na amani ya akili ili kufikia malengo yao ya kimaada na kiroho.

Wasiwasi na woga ni vikwazo vikubwa katika njia ya kufikia amani na utulivu. Na moja ya mambo ambayo husababisha wasiwasi na woga ni haraka ambayo ni hasi.

Kuwa na haraka au hamaki ni miongoni mwa sifa za kusikitisha zinazopelekea majuto. Kufanya kila kitu kunahitaji maandalizi na utangulizi na kutozingatia nukta hizo huwa na madhara.

Ili tufaha kuiva, linahitaji kupitia hatua kadhaa kuanzia kupatikana mbegu hadi kupandwa, kuppata maji ya kutosha, kupaliliwa, n.k. Ikiwa hatua hizo hazitachukuliwa ipasavyo  na mtu akaingia hatua za haraka haraka, matokeo yatakuwa mabovu na mti hautakuwa na mazao.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 37 ya Surah Al-Anbiya: “Mwanaadamu ameumbwa na haraka. Nitakuonyesheni Ishara zangu. Basi msinihimize".

Kufanya jambo lolote kunahitaji mambo mawili, kwanza kuwa na nishati na uwezo wa kutumia nishati inayohitajika kwa ajili yake na, pili, kuwa na nishati ya akili na motisha.

Waswahili wana msemo maarufu wa haraka haraka haina baraka ambao kimsingi una chimbuko katika mafundisho ya Kiislamu.

Kuwa na haraka husababisha wote wawili kutofanya kazi. Kuwa na haraka husababisha kupoteza nguvu na uwezo wa mtu na kile kinachofanywa hakitakuwa na matokeo ya kuhitajika.

Kwa hivyo, kukimbilia na kuharakisha mara nyingi husababisha majuto.

Ndio maana Imam Ali (AS) anasema: “Wale wanaokimbilia kupata kitu watakuwa na majuto watakapokipata na kutamani wasingelikipata. (Khutba ya 150 ya Nahj al-Balagha)

Bila shaka, kunapaswa kuwa na tofauti kati ya haraka na kasi. Kufanya haraka ni kufanya jambo kabla ya maandalizi muhimu, wakati kuwa na kasi ni kufanya kazi kwa kasi ipasavyo baada ya maandalizi kufanyika.

captcha