IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu / 25

Maadili; Pendekezo Kuu la Mtume Muhammad (SAW) na Imam Hussein (AS)

12:47 - September 03, 2023
Habari ID: 3477541
TEHRAN (IQNA) – Tunaposoma kauli za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na Imam Hussein (AS), tunaona kuna kiwango kikubwa cha mapendekezo kuhusu masuala ya maadili katika matamshi ya watukufu hao wawili.

Hii inaonyesha kwamba dini sio tu kuhusu masuala ya msingi kama kumuamini Mwenyez Mungu mmoja bali maadili pia yana nafasi kubwa katika dini.

Kimsingi, dini inadhihirika kwa imani kwa imani na kwa vitendo kwa maadili.

Ipo Hadith kutoka kwa Imam Ali (AS) kwamba iliposhuka Aya ya kwanza ya Sura An-Nasr, Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) hakutoka nje ya nyumba yake kwa siku kadhaa na kisha siku ya Alhamisi, alimuamuru Bilal (RA) aadhini ili  kila mtu aende msikitini kwa sababu Mtume (SAW) alitaka kutoa kauli.

Baada ya waumini kukusanyika msikitini, Mtume (SAW) alianza kwa kusema kwamba alikuwa na hamu sana ya kwenda kwa Mwenyezi Mungu lakini alikuwa na huzuni kwa sababu angewaach waumini. Kisha akasema, "Kuna maneno yangu ya mwisho kweny katika ulimwengu huu."

Maneno na mapendekezo ya mwisho ya Mtume (SAW) yalikuwa kuhusu dini, haja ya kuwa mwaminifu na haja ya kuheshimu haki za wengine, wakiwemo wanafamilia.

Amesema mtu akiwadhulumu wale walio chini yake, Mtume (SAW) atakuwa adui yake Siku ya Kiyama. “Msiwadhulumu wanawake, na mkiwadhulumu, wema wowote mlio nao utaharibika Siku ya Kiyama. Kuwa mwangalifu (kuheshimu haki za wanafamilia). Wafundishe adabu na hulka njema.”

Maneno haya ni muhimu sana hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba ni maneno ya mwisho ya Mtukufu Mtume (SAW) kwa watu.

Kisha akawataka watu wawapende Ahl-ul-Bayt wake (AS), Qur'ani Tukufu na wanachuoni wa Umma. Pia alitoa ushauri juu ya umuhimu wa kuswali na kutoa Zaka.

Mtume (SAW) pia alionya dhidi ya dhulma na kutenda madhambi, akisisitiza umuhimu wa Taqwa (kumcha Mungu).

Kisha akaenda nyumbani na kukaa huko hadi wakati wa kifo chake.

Kwa hiyo jambo kuu katika matamshi ya mwisho ya Mtukufu Mtume (SAW) lilikuwa ni kuhusu masuala ya maadili.

Tunaona maneno na mapendekezo yale yale katika kauli za Imam Hussein (AS).

Huko Karbala na wakati wa mapambano, Imam Hussein (AS) alikuwa akiuliza kuhusu hali za masahaba zake na kila wakati alipokuwa akifahamishwa kuhusu kifo chao cha kishahidi hadi Imam Sajjad (AS) alipomwambia Imam Hussein (AS) kwamba hakuna watu waliosalia jeshini isipokuwa wawili tu.

Katika hali kama hiyo, Imam Hussein (AS) alitoa pendekezo lake la mwisho, ambalo lilikuwa juu ya kuwa mkarimu kwa wengine, wakiwemo wanafamilia.

Hivyo, tunaona kuna kiasi kikubwa cha mapendekezo kuhusu masuala ya maadili katika matamshi ya Mtukufu Mtume (SAW) na Imam Hussein (AS).

Hii ni dalili kwamba dini sio tu kuhusu masuala ya msingi kama imani ya Mungu mmoja bali maadili pia yana nafasi kubwa katika dini.

captcha