IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /13

Qur'ani Tukufu inasisitiza kuepuka kushuku au dhana mbaya

16:17 - July 19, 2023
Habari ID: 3477308
TEHRAN (IQNA) – Aya nyingi za Qur'ani zinataja masuala ya kimaadili na kutoa ushauri wa kimaadili. Moja ya mashauri haya ni kuepuka kuwashuk au kuwadhania vibaya watu.

Kuwa na dhana mbaya au kuwashuku  wengine ni hisia ambayo husababisha mmomonyoko wa imani katika jamii na kudhoofisha misingi ya jamii. Mtu hutenda kulingana na jinsi anavyofikiri na tabia yake ni kiakisi cha mawazo yake. Kuwa na mawazo mabaya juu ya wengine husababisha mtu kuwa na tabia isiyofaa kwao.

Qur’ani Tukufu, ambayo ni kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye anajua yote kuhusu fikra na tabia za binadamu, inakataza kuwa na shaka: “ Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu." (Aya ya 12 ya Surah Al-Hujurat)

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anakataza dhana au kuwashuku wengine na kusema ni utangulizi wa kusengenya. Mtu anaweza kuuliza kwa nini Mwenyezi Mungu anasema epuka dhana nyingi. Ni kwa sababu tuhuma dhana nyingi huibua tuhuma zisizo na msingi.

Tuhuma mbaya ni za aina mbili. Mengine yanatokana na ukweli na mengine hayana msingi. Kuwa na tuhuma zisizo na msingi ni dhambi na kwa sababu mtu hawezi kuwa na uhakika ni zipi zinazoegemezwa kwenye ukweli na zipi sio, anapaswa kuepuka tuhuma mbaya kabisa.

Katika aya nyingine, Quran inarejelea aina nyingine ya dhana mbaya, ambayo ni kuhusu Mwenyezi Mungu: “Na awape adhabu wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanao mdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Mwenyezi Mungu awakasirikie, na awalaani, na awaandalie Jahannamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa." (Aya ya 6 ya Surah Al-Fat’h)

Shaka ambayo baadhi ya Waislamu walikuwa nayo ni kwamba walifikiri ahadi za Mwenyezi Mungu kwa Mtukufu Mtume (SAW) hazitatokea kamwe na Waislamu hawatawashinda maadui na hawatarejea Madina. Na makafiri walidhani kwamba Mtume (SAW), ambaye alikuwa na masahaba wachache na silaha chache, atashindwa na Uislamu utatoweka hivi karibuni. Lakini  Mwenyezi Mungu alikuwa ameahidi ushindi wa Waislamu na ndivyo ilivyokuwa.

Qur'anI Tukufu inapiga marufuku tuhuma hizo na kusema wale wanaoziunga mkono  watapata adhabu chungu.

captcha