IQNA

Maadili katika Qur'ani / 11

Kusengenya ni dhambi kubwa

23:20 - July 10, 2023
Habari ID: 3477264
TEHRAN (IQNA) – Kusengenya ni tabia isiyofaa inayoathiri vibaya jamii. Ni dhambi kubwa ambayo Qur'ani Tukufu imewatahadharisha waumini wajiepuke nayo.

Ni mbaya sana kuharibu mahusiano ya watu wao kwa wao na njia moja ya kufanya hivyo ni kusengenyana. Kwa kifupi, kusengenya ni kumwambia mtu kuhusu matamshi ya faragha ya mtu mwingine kwa lengo la kuvuruga uhusiano kati ya watu hao wawili.

Qur'ani Tukufu imeitaja  tabia hii na inamuamuru Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) aepuke kuzingatia matamshi kama hayo:

“Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. (kusengenya na kusengenyana)” (Aya ya 10-11 ya Surah Al-Qalam)

Kurejelea kitendo cha kusengenya pamoja na madhambi mengine makubwa kunaonyesha jinsi lilivyo kubwa. Watu wanaofanya dhambi hii ni wale wanaotoka kuwafanya watu wasiaminiane wao kwa wao na kupanda mbegu za uadui baina yao, jambo ambalo ni miongoni mwa madhambi makubwa.

Jambo la kielimu katika Aya hii ni kwamba mtu yeyote asiwaamini watu waliozoea kusengenya. Watu kama hao wanapaswa kukataliwa katika jamii.

Ikiwa pande zote mbili zinazozozana zinasikiliza na kuzingatia anachosema mchongezi, kuna uwezekano mkubwa wa kujuta.

captcha