IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /17

Tabia zinazoharibu mtaji wa kijamii

22:29 - August 07, 2023
Habari ID: 3477395
TEHRAN (IQNA) – Nguzo kuu ya kuhifadhi jamii, iwe kubwa au ndogo, ni uaminifu. Ikiwa uaminifu utapotea, jamii itakabiliwa na kila aina ya madhara ambayo yanaweza kudhoofisha msingi wake.

Lakini ni mambo gani yanaweza kudhoofisha uaminifu na kuharibu mtaji huu wa kijamii?

Mmoja ya mambo hayo ni kusengenya. Ni dhambi kubwa ambayo Hadithi zimeonya vikali dhidi yake. Kusengenya kunamaanisha kuzungumza kwa nia mbaya juu ya mtu ambaye hayupo.

Quran inatoa mfano kuonyesha jinsi kusengenyana kulivyo mbaya. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 12 ya Surah Al-Hujurat: “2. Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu."

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu anafananisha kusengenya na kula nyama ya ndugu aliyekufa. Hii ni kwa sababu mtu ambaye anasengenywa hayupo na hawezi kujitetea, kama vile mtu aliyekufa hawezi kujitetea..

Mtu anayejihusisha na usengenyaji ni mtu dhaifu na mjinga ambaye hana ujasiri wa kukabiliana na masuala na hivyo kumshambulia ndugu yake aliyekufa.

Mtu anayezoea kusengenya pia huwa na mashaka na watu wote na hutumia nguvu na wakati wake wote kugundua nukta za giza za wengine ili kuweza kuchafua taswira yao.

Kwa njia hii, anadhoofisha imani ya umma na kumomonyoa misingi ya jamii.

Kwa kawaida, mtu anayesema vibaya juu ya wengine mbele yako ana uwezekano mkubwa wa kusema vibaya juu yako wakati haupo pia. Ndio maana mafundisho ya dini yanatuhimiza tusisikilize masengenyo na tusiruhusu mtu yeyote afanye uovu huo mbele yetu.

Uponyaji kuu wa ugonjwa wowote wa mwili na kiakili ni kutafuta sababu kuu ya ugonjwa na kuiondoa. Chanzo kikuu cha kusengenya ni masuala kama vile husuda, chuki, majivuno, ubinafsi, na hila na ikiwa tabia hizi mbaya hazitang'olewa, mtu hawezi kutumaini kuwa ataweza kuachana na usengenyaji.

captcha