IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /24

Moto unaounguza kila kitu katika njia yake

18:09 - August 30, 2023
Habari ID: 3477521
TEHRAN (IQNA) – Kufr ni neno la Kiarabu lenye maana ya kufunika na kukanusha ukweli na kwa hakika Kufr ina madhara makubwa kwa watu binafsi na jamii.

Kupambana na aina mbalimbali za magonjwa na matatizo ya kifedha ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili watu wote maishani. Changamoto hizi zinaweza kuwa majaribu kwa watu kwa sababu Mwenyezi Mungu anataka kuwajaribu. Wakati mwingine hutokea kama matokeo ya kutokuwa na shukrani kwa baraka za awali ambazo mtu amepokea. Kama vile shukrani huleta baraka nyingi zaidi, ukosefu wa shukran pia husababisha kupoteza baraka.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 28 ya Surah Al-Baqarah: " Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake mtarejeshwa?."

Aya hii inasisitiza kwamba mwanadamu ambaye ni kiumbe dhaifu hapaswi kukataa kuwepo kwa Muumba ambaye hahitaji mtu yeyote na chochote. Baadhi ya mafunzo ambayo mtu anaweza kujifunza kutokana na aya hii ni kama ifuatavyo:

  • Kufr ni neno la Kiarabu lenye maana ya kufunika na kukanusha ukweli. Wakati fulani mkulima huitwa Kafir kwa sababu anaficha mbegu kwenye udongo. Kafir (kafiri) ni mtu ambaye anaficha thamani ya baraka zinazotolewa na Mungu au anajaribu kuficha uwepo wa Mungu.
  • Qur'ani Tukufu inatukumbusha sisi sote kwamba tulikuwa viumbe visivyo na uhai kama mbao na tukajaaliwa baraka za uhai. Tumepewa ubongo, macho, masikio na viungo na tumebarikiwa kuwa na akili na ufahamu. Basi inakuwaje tunaelekea Kufr na kukana uwepo wa Mungu?
  • Njia bora ya kumjua Mungu ni kutafakari juu ya uumbaji wetu na uumbaji wa ulimwengu. Kufikiri juu ya uumbaji, uhai na kifo kutatuongoza kwenye hitimisho kwamba maisha yetu hayatokani na sisi wenyewe. Ingekuwa hivyo, tungeishi milele, lakini ukweli ni kwamba uhai unatolewa kwetu (na Mungu) na kisha kuchukuliwa kutoka kwetu.

Mwenyezi Mungu amewakadhibisha wale wanaoishi katika ukafiri na wakafa katika ukafiri: “Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu yao laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote." (Aya ya 161 ya Surah Al-Baqarah)

captcha