IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /22

Ghaflah huharibu alichonacho mwanadamu

21:13 - August 26, 2023
Habari ID: 3477501
TEHRAN (IQNA) – Ghaflah, neno la Kiarabu lenye maana ya kupuuza, kughafilika, na kusahau, ni tabia yenye madhara ambayo huharibu matendo mema ya mtu.

Kuelewa aina tofauti za Ghaflah na jinsi inavyoathiri maisha ya mtu katika dunia hii na ijayo ni muhimu sana.

Kuna aya nyingi za Qur'ani Tukufu zinazotaja Ghaflah, na hii ni dalili ya jinsi ilivyo muhimu kukabiliana nayo.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 146 ya Surah Al-A’raf: “Nitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu wamezikanusha Ishara zetu, na wameghafilika nazo.”

Ghaflah ni dhana ambayo ina upeo mpana na inajumuisha kila aina ya kupuuza na kughafilika kuhusu dunia na akhera.

Moja ya matokeo ya Ghaflah ambayo ni hatari sana ni kwamba inaharibu juhudi na matendo ya mtu.

1- Kuharibu juhudi katika ulimwengu huu:

Wakati mwingine mtu ambaye anakabiliwa na matatizo mengi katika maisha hufanya jitihada nyingi za kukusanya mtaji lakini anapoteza yote kwa kupuuza kidogo. Haya ni matokeo ya kidunia ya Ghaflah ambayo huharibu juhudi zote za mtu.

2- Ghaflah inayoharibu athari za matendo mema huko akhera

Kwa mujibu wa Ayatullah Makarem Shirazi, aina hii ya Ghaflah huharibu matendo ya mtu. Wale wanaoteseka kutokana na Ghaflah ni nadra sana kufanya matendo mema na wakifanya, Ghaflah yao haiwaruhusu kufanya jambo jema kwa Ikhlas (nia safi).

Imam Ali (AS) amesema: Jiepusheni na Ghaflah na kiburi kwa sababu Ghaflah inaharibu matendo ya mtu.

captcha