IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /19

Kusema Uongo; Uovu wa unaosababisha mwandamu kuishia motoni

10:40 - August 14, 2023
Habari ID: 3477433
TEHRAN (IQNA) – Miongoni mwa viungo vya mwili, ulimi ni moja ambayo kwayo madhambi mengi yanaweza kutendwa.

Moja ya madhambi makubwa yanayofanywa kwa ulimi ni kusema uwongo na ni dhambi ambayo inaweza kusababisha madhambi mengine pia.

Ili kuelewa vipengele mbalimbali vya kila tendo, tunapaswa kupata motisha nyuma yake. Qur'ani Tukufu inaashiria sababu ya kusema uwongo katika Aya ya 105 ya Surah An-Nahl: “Wanao zua uwongo ni wale tu wasio ziamini Ishara za MwenyeziMungu. Na hao ndio waongo.".

Ikiwa mtu anamwamini Mwenyezi Mungu, uwezo Wake na ujuzi Wake, na ahadi Zake, hawezi kamwe kusema uwongo ili kupata mali au vyeo au mali nyinginezo za kidunia. Haogopi umaskini au kupoteza heshima au cheo na kamwe hasemi uwongo ili kubakia katika nafasi ya cheo.

Jambo muhimu kuhusu kusema uwongo ni kwamba si dhambi tu bali pia ni tendo linaloweka msingi wa dhambi nyingine.

Imam Hassan Askari (AS) alisema kuwa maovu yote yamefungwa kwenye chumba na ufunguo wake ni uongo.

Wenye dhambi wanapohisi kutishwa na kuogopa fedheha, wanaanza kusema uwongo ili kufunika dhambi zao. Kwa maneno mengine, kusema uwongo kunawaruhusu kufanya aina tofauti za dhambi bila kuogopa kwamba dhambi zao zinaweza kufichuliwa.

Hata hivyo, mtu mkweli huepuka dhambi kwa sababu anajua kwamba hawezi kusema uwongo ili kuzificha.

Mwenyezi Mungu katika aya tofauti za Qur'ani Tukufu amewaonya watu dhidi ya kusema uwongo, akisisitiza kwamba waongo hawatapata furaha:

"Sema: Hao wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.” (Aya ya 69 ya Sura Yunus).

captcha