IQNA

Maadili katika Qur'ani Tukufu /18

Kuwa bakhili humfanya mtu kuwa mpweke

16:01 - August 09, 2023
Habari ID: 3477405
TEHRAN (IQNA) – Hata kama wana familia kubwa au marafiki wengi, baadhi ya watu hujikuta wapweke zaidi duniani kwa sababu ya tabia zao, mojawapo ikiwa ni ubakhili.

Mwenyezi Mungu anataja Bukhl (ubakhili) katika aya nyingi za Qur'ani Tukufu. Wakati fulani Mwenyezi Mungu huwapa baadhi ya watu baraka ambazo ni zaidi ya kile wanachohitaji ili waweze kusambaza neema na Baraka walizotunukiw kwa wengine. Wakikataa kufanya hivyo, basi watakuwa ni mabakhili.

Mwenyezi Mungu anakemea hili katika aya nyingi na wakati mwingine anaonya kwamba adhabu katika moto wa Jahannamu inawangoja wale ambao ni mabakhili.

 Wala wasidhani wale ambao wanafanya ubakhili katika aliyo wapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni kheri yao. Bali hiyo ni shari kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyo yafanyia ubakhili Siku ya Kiyama. Na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote myatendayo.” (Aya ya 180 ya Surah Al-Imran)

Sababu kuu ya mambo kama ubakhili ni ukosefu wa imani kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa mtu anamchukulia Mwenyezi Mungu kuwa muweza wa yote, anapaswa kutambua kwamba wema wote na baraka zote zinatoka kwake.

Ikiwa mema yote na baraka zote zinatoka kwa Mungu, basi tunapaswa kuamini ahadi zake na kujua kwamba tukitumia fedha zetu kwa ajili ya jambo jema na kuwasaidia wengine, Mwenye Mungu atatuzidishia na kutupa baraka nyingi zaidi.

Imam Ali (AS) anasema kwamba sababu ya baadhi ya watu kuwa ubakhili ni kwa sababu wana shaka juu ya uwezo wa Mwenyezi Mungu na ahadi zake.

Ubakhili  sio tu juu ya mali na pesa. Baadhi ya watu wana ubakhilo linapokuja suala la kuwapa wengine maarifa, ujuzi au elimu. Wengine hata wana ubakhili katika kuwasalimia wengine. Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alisema mtu bakhili zaidi ni yule ambaye ana ubakhili katika kuwasalimia wengine.

Kwa kawaida, ikiwa mtu ana ubakhili, atapoteza marafiki zake na masahaba na kuwa mpweke.

Kwa hiyo moja ya matokeo ya wazi kabisa ya kuwa bakhili ni kuwa mpweke kwa sababu mtu wa namna hiyo anajitakia baraka zote na kila jema na hajali wengine. Hivyo, wengine wanatambua kwamba hakuna jema lolote kutoka kwake litakalowafikia na hivyo kumuacha. Ndio maana Imam Ali (AS) anasema kwamba bakhili hana marafiki.

captcha