IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Msomi wa Bangladesh: Kufuata mafundisho ya Qur'ani ni muhimu ili kujenga Ustaarabu Mpya wa Kiislamu

15:03 - February 21, 2024
Habari ID: 3478390
IQNA - Mtaalamu wa Qur'ani wa Bangladesh amesisitiza haja ya kukimbilia Qur'ani Tukufu ili kuunda ustaarabu mpya wa Kiislamu.

"Sote lazima tugeukie Qur'ani na kufuata mafundisho yake," Ahmed bin Yusuf al-Azhari, ambaye ni mjumbe wa jopo la majaji wa Awamu ya 40  ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ameliambia meliambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) katikla mahojiano pembezoni mwa mashindano hayo yanayomalizika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Tehran.

"Tunapaswa kufundisha Qur'ani kwa watoto kutoka umri mdogo na kuanza kuifahamisha jamii kuhusu utamaduni wa Kiislamu kuanzia shuleni," aliongeza.

"Hivyo ndivyo tunavyoweza kuifanya jamii ya baadaye kuwa ya Kiislamu na kuanzisha ustaarabu mpya wa Qur'ani na Kiislamu."

Alipoulizwa kuhusu shughuli zake za Qur'ani, al-Azhari alisema anahudumu kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani inayojulikana kama Taasisi ya Kimataifa ya IQRA.

Alisema alijifunza Quran kwa kuhimizwa na baba yake na alisoma katika shule ya Kiislamu.

Mnamo 2002, alikwenda Misri na kusoma katika Kituo cha Al-Azhar's Qara'at kwa miaka minane, akifaidika na utaalamu wa maustadhi kama Sheikh Raghib Mustafa, Sheikh Abdul Ati Nasif na Sheikh Nabil.

Kisha akarudi Bangladesh na kuanza kufundisha Quran katika nchi yake.

Alisema baba yake, Sheikh Yusuf,  alikuwa qari mashuhuri katika historia ya Bangladesh na Pakistan (Kuanzia 1947 hadi 1971 Bangladesh na Pakistan zilisimamiwa na serikali moja).

"Baba yangu alizindua duru na programu za Qur'ani nchini Bangladesh na kuwaalika maqari mashuhuri wa Misri kama Sheikh Abdul Basit Abdul Samad, Sheikh al-Husari na Sheikh Kamil Yusuf al-Bahtimi.

Alibainisha kuwa kutokana na juhudi za baba yake, vituo vingi vya Qur'ani vilianzishwa nchini Bangladesh, maqari wengi walipata mafunzo, na programu nyingi za kimataifa za Qur'ani zilifanyika nchini humo.

Baada ya kifo cha baba yake, al-Azhari akawa Sheikh-ul-Qurra (qari wa juu) wa Bangladesh.

Kwingineko katika matamshi yake, al-Azhari ameashiria mafungamano ya kitamaduni ya muda mrefu kati ya Iran na Bangladesh na kusema watu wa nchi yake wanaipenda Iran na wanawajua maqari wengi mashuhuri wa Iran na wanapenda kusikiliza qiraa zao.

4200894

Habari zinazohusiana
captcha