IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

Waziri Esmaili: Iran inajulikana kwa harakati kubwa ya Qur'ani Tukufu

13:06 - February 16, 2024
Habari ID: 3478359
IQNA-Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema, ujumbe wa Qur'ani ni ujumbe wa Muqawama na Jihadi na kuongeza kuwa, Iran inajulikana kwa harakati kubwa ya Qur'ani.

Mohammad Mehdi Esmaili ameyasema hayo Alhamisi jioni jijini Tehran katika hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya 40 ya Kitaifa ya Qur'ani na Mashindano ya nane ya Qur'ani ya Wanafunzi wa Ulimwengu wa Kiislamu.

Esmaili ameeleza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajulikana kutokana na harakati kubwa ya Imamu Khomeini (MA) ambayo ni harakati ya Qur'ani na akaongeza kuwa, ujumbe wa Qur'ani Tukufu ni ujumbe wa Muqawama na Jihadi, na leo tunashuhudia kupata nguvu na kutukuka Jihadi na Muqawama katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema, "leo wananchi wa Gaza wanaandamwa na mashambulio na hujuma kali zaidi za utawala wa Kizayuni kwa zaidi ya miezi minne, lakini watoto waliopoteza familia zao wanasimama kwa uimara na ujasiri mbele ya kamera na kuzungumzia Muqawama. Hii ni Qu'rani ambayo imeifanya anga ya Muqawama kuwa hivyo".

Duru ya 40 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani na mashindano ya nane ya Qur'ani ya wanafunzi wa Ulimwengu wa Kiislamu yenye kauli mbiu "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja, Kitabu cha Muqawama" yameanza rasmi hapa mjini Tehran katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano kwa kuhudhuriwa na Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Bunge na maafisa kadhaa wa kitaifa na wasimamizi wa masuala ya Qur'ani hapa nchini.

Nchi zinazoshiriki katika mashindano ya mwaka huu yatakayofikia kilele tarehe 21 Februari ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Malaysia, Misri, Algeria, Saudi Arabia, Uturuki, Indonesia, Lebanon, India, Uholanzi, Ujerumani, Marekani, Tunisia, Russia, Ivory Coast, Sri Lanka, Singapore, Senegal, Syria, Iraq, Canada, Palestina, Ufilipino, Jordan, Pakistan, Comoro, Burundi, Libya, Afghanistan, Niger, Somalia, Bangladesh, Tanzania, Mauritania, Thailand, Tajikistan, Uingereza, Nigeria, Ethiopia, Uganda, Oman, Brunei, Gambia na New ,

4200063

Habari zinazohusiana
captcha