IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu / 17

Qur'ani; Kitabu Kitukufu

21:50 - July 24, 2023
Habari ID: 3477332
TEHRAN (IQNA) – Qur'ani Tukufu inajitambulisha kama “Quran al-Majid” (Qur’ani Tukufu).

Haya ni baadhi ya maelezo ya Kitabu kitakatifu yaliyotajwa katika aya kadhaa:

“Qaaf. Naapa kwa Qur'ani Tukufu!" (Aya ya 1 ya Surah Qaaf)

“Hakika hii ni Qur’ani Tukufu iliyomo ndani ya kibao kilicho hifadhiwa. (Aya 21-22 ya Surah Al-Buruj)

Majid ni neno ambalo mzizi wa neno lake ni Majd, lenye maana ya utukufu uliompana na Qur'ani Tukufu ni pana na ina utukufu usio na kikomo. Ni Kitabu Kizuir na yaliyomo ni makubwa sana, amri zake ni bora na mafundisho yake ni yenye uhai.

Wafasiri wa Qur'ani Tukufu wametaja mambo ya kuvutia kuhusu Aya ya 1 ya Surah Qaaf:

1- Kuapa kwa Qur'ani Tukufu ni muhimu sana kwa sababu ina utukufu na ukuu. Katika aya nyingi za Kitabu kitukufu, Mwenyezi Mungu anaapa kwa vitu tofauti kama vile Dhat (dhat (asili) yake), Siku ya Kiyama, Malaika, jua, mwezi, n.k. Mwenyezi Mungu hahitaji kuapa kwa chochote ila viapo vilivyomo ndani ya Qur'ani Tukufu vina manufaa mawili makubwa. Kwanza, wanatilia mkazo juu ya kile kitakachosemwa na, pili, wanaonyesha ukuu wa kile ambacho Mungu anaapa nacho. Hakuna anayeapa kwa kitu kisicho na thamani.

Ushahidi mmoja wa ukweli kwamba Al-Huruf al-Muqatta'a (herufi zilizotengana) ndani ya Qur'ani Tukufu ni kuonyesha ukuu wa Kitabu kitukufu ni kwamba katika Surah Qaaf, Mungu anaapa kwa "Qur'ani Tukufu" mara tu baada ya herufi iliyojitenga.

2- Ukitaka utukufu na ukuu unatakiwa uende kwa mwenye utukufu na ukuu. Ikiwa mtu anataka kuishi maisha ya heshima, anapaswa kuishi na kushirikiana na watu wenye heshima. Ndio maana Mungu anasema ukitaka ukuu na utukufu uende kwenye Quran.

3- Iwapo Qur'ani Tukufu ni Majid na Kareem, basi tunapaswa kuitukuza na kuiheshimu. Mwenyezi Mungu anapoielezea Qur'ani Tukufu kuwa ni tukufu na yenye heshima, inatuongezea wajibu wa kukitukuza na kukiheshimu Kitabu kitukufu.

Ama katika Aya ya 21-22 ya Sura Al-Buruj, Mwenyezi Mungu anaielezea Qur'ani Tukufu kuwa ni Majid ili kusisitiza kwamba msisitizo wa makafiri wa kuikataa na kuitaja kuwa ni uchawi na ushairi ni bure kwa sababu Qur'an ni tukufu na inalindwa kwa kibao kilichohifadhiwa vizuri, kwa hivyo maovu hayawezi kuifikia na kuipotosha.

captcha