IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu/5

Qur'ani Tukufu, Kitabu cha ukumbusho (dhikr) na mawaidha

21:44 - June 10, 2023
Habari ID: 3477128
Kwa mujibu wa aya katika Qur'ani Tukufu, Kitabu kitukufu kilitumwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaamsha watu na maana ya mwamko huu inapatikana katika aya nyingine.

Neno Dhikr (kukumbusha) limetumika katika aya kadhaa kuelezea Qur'an Tukufu, ikiwa ni pamoja na katika Aya ya 17 ya Surah Al-Qamar: " Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?

Kukumbusha na kutoa nasaha ni mambo ambayo Qur'ani inaangazia kutokana na manufaa yake kwa waumini.

Kuitafakari aya hii kunadhihirisha mambo mengi, yakiwemo yafuatayo:

Msisitizo juu ya suala la Dhikr. Katika Qur'ani Tukufu, Dhikr ina nafasi maalum, kwani inaamsha na kuhuisha nyoyo na kuteka fikira kwenye ukweli. Kuna watu ambao wako tayari kuukubali ukweli na wanapopewa ushauri na kukabiliana na Dhikr, huipata kwa urahisi ukweli na kutembea kwenye njia yake.

Bila shaka kuna wengine ambao hufurahishwa na shangwe za muda mfupi na wanapoona mapendezi yao yakiwa hatarini, wanachukua msimamo dhidi ya kweli. Wanapokabiliana na Dhikr, baadhi ya watu hawa hugeuka hatua kwa hatua kwenye njia ya ukweli huku kukiwa bado na baadhi ya wanaosisitiza kuendelea na njia yao ya awali.

Je, Qur'ani Tukufu inatumia njia gani kwa Dhikr? Njia mojawapo ni kuwakumbusha watu kifo. Kifo ni jambo litakalotokea kwa viumbe vyote. Qur'an mara kwa mara inazungumza kuhusu kifo na vipengele vyake tofauti ili kuwaamsha watu na kuwakumbusha juu ya mwisho wa maisha ya dunia.

"Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kaamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.” (Aya ya 185 ya Surah Al Imran)

Moja ya matokeo ya kukumbuka kifo ni kwamba mtu anatambua kwamba siku moja ataondoka duniani na atalazimika kuwajibika kwa matendo yake katika kila sekunde ya maisha haya. Hili litamfanya awe mwangalifu zaidi katika yale anayoyafanya na kuepuka kufanya jambo ambalo litamfanya ajutie matendo yake huko akhera.

captcha