IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu / 16

Kitabu Ambacho hakuna mtu apasaye Kukigusa Isipokuwa waliotakaswa

11:46 - July 22, 2023
Habari ID: 3477320
TEHRAN (IQNA) - Kwa sababu kitabu hiki kina manufaa mengi kwa ubinadamu na kinawaongoza watu kwenye njia iliyo sawa, kuwajua wale wanaoweza kuufikia ukweli wake kuna umuhimu mkubwa.

Katika Surah Al-Waqi’a, Mwenyezi Mungu anarejea kwenye moja ya sifa za Qur'ani Tukufu na kusema kufikia ukweli wake ni kwa ajili ya kundi fulani tu la watu. “Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu. Katika Kitabu kilicho hifadhiwa.” (Aya ya 77-79 ya Surah Al-Waqi’a)

Kuna mambo mawili yanayojadiliwa kuhusu ‘waliotakaswa’ yaliyotajwa katika aya hii:

  • Usafi wa Nje: Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, ibara ya “usiguse isipokuwa waliotakaswa” ina maana kwamba watu lazima wafanye Wudhu kabla ya kugusa aya za Kitabu kitukufu kwa sababu Wudhu huleta usafi wa mwili na roho na una athari kubwa chanya kwenye akili na roho ya watu.

Imamu Ridha (AS) amesema: “Mwenyezi Mungu ametuamrisha kufanya Wudhu kisha tuanze Swala ili mtu huyo awe msafi na mtiifu kwa amri Yake na awe mbali na uchafu anaposimama kuswali mbele yake.

Kwa kuzingatia aina hii ya Hadithi, watu wote wanaweza kugusa Qur'anI Tukufu mradi tu wamewahi kufanya Wudhu kabla.

  • Usafi wa ndani: Usafi wa namna hii ni kwa ajili ya watu fulani tu na haujumuishi watu wote.

Katika Aya ya 33 ya Surah Al-Ahzab, Mwenyezi Mungu anawatambulisha wale waliotakaswa: “…Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara. Imepokewa kwamba siku moja Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alikuwa amelala na joho juu yake kisha Bibi Zahra (SA) aliingia ndani ya nyumba akiwa na sahani mkononi mwake. Mtume (SAW) akamwambia amuite mumewe na wanawe wawili. Walipokuja na kuanza kula sahani pamoja, aya hii ilifunuliwa: “Enyi watu wa nyumba, Mungu anataka kuwaondoleeni kila aina ya uchafu na kuwatakasa kabisa. Mtukufu Mtume (SAW) aliwafunika kwa joho na akasema mara tatu: “Ewe Mola! Hawa ndio watu wa nyumbani mwangu, waondolee uchafu na uwatakase”

Kwa mujibu wa Hadithi hii na nyinginezo, Ahl-ul-Bayt (AS) ni Maasumin 14 ambao Mungu Amewatakasa. Kwa hiyo Ahl-ul-Bayt (AS) ndio waliotakasika ambao wamefikia ukweli wa Qur'ani na hakuna yeyote isipokuwa wao anayeweza kufikia ukweli wa Qur'ani Tukufu.

captcha