IQNA

Hija 1444

Mahujaji watembelea kiwanda cha kuchapisha Qur'ani Tukufu cha Madina

15:52 - July 04, 2023
Habari ID: 3477234
MEDINA (IQNA) – Baadhi ya Mahujaji ambao wamesafiri kwenda Madina baada ya ibada ya Hija kutembelea jengo la uchapishaji la Qur’ani Takatifu katika mji huo mtakatifu.

Wametembelea Kituo cha Mfalme Fahd kwa Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu ndani ya mpango uliozinduliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, Dawah, na Mwongozo.
Mahujaji wamejifunza kuhusu hatua mbalimbali za uchapishaji wa Qur'ani Tukufu, tafsiri katika lugha mbalimbali, kusahihisha na kuhariri, na usambazaji wa nakala za Qur'ani Tukufu.

Wale wanaotembelea kiwanja hicho pia wamejaliwa nakala za Kitabu Kitakatifu na tafsiri zake. Kituo cha Mfalme Fahd cha Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu kiko katika mji mtakatifu wa Madina. Kituo hicho kinachapisha takriban nakala milioni 20 za Qur'ani Tukufu kila mwaka. Pia huchapisha tafsiri za Kitabu Kitakatifu katika lugha mbalimbali.

Hajj Pilgrims Visit Medina Quran Printing Complex

4152138

Kishikizo: Hija 1444
captcha