IQNA

Ibada ya Hija 1444

Waislamu waendelea kumiminika Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Hija + Video

Makka,, mji mtakatifu zaidi katika Uislamu, unaendelea kukaribisha Waislamu wanaofika katika mji huo kwa ajili ya ibada ya kila mwaka ya Hija.

Ifuatayo hapa ni ripoti ya mwandishi wa Press TV akiripoti kutoka Makka.

Hivi karibuni Wizara ya Hija na Umra ya Saudi Arabia ilitoa taarifa ya miongozo jumla kwa Mahujaji wa mwaka huu wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa lengo la kurahisisha ibada hiyo.
Ibada ya Hija ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waislamu, ambao hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Dhul-Hijjah katika mji mtakatifu wa Makka na kandokando yake nchini Saudi Arabia.
Katika taarifa yake hiyo, Wizara ya Hija na Umra ya Saudia imesema, ili kurahisisha masuala ya kiidara yanayohusiana na safari, mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu wabebe hati zao rasmi hasa zinazohusiana na amali za Hija na kuchukua mizigo mepesi wakati wa utekelezaji wa amali za Hija.
Inakadiriwa kuwa mwaka huu, Saudi Arabia itapokea Mahujaji zaidi ya milioni mbili, kiasi kwamba mashirika ya ndege ya nchi hiyo yameshatenga tiketi zaidi ya 1,200,000 kwa ajili ya wageni wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. Viwanja sita vya ndege vya ndani ikiwa ni pamoja na Jeddah, Riyadh, Al-Dammam, Madinatul-Munawwara, Al-Taif na Yan'ba vitapokea ndege zitakazobeba mahujaji wa mwaka huu.
Kishikizo: Hija 1444 ، hija