IQNA

Ibada ya Hija 1444

Msafara wa Qur'ani wa Iran waeneza Umoja wa Waislamu katika vikao vya Qur'ani huko Makka + Video

22:01 - June 10, 2023
Habari ID: 3477129
Kundi la maqari (wasomaji Qur'ani Tukufu) wa Iran huko Makka nchini Saudi Arabia katika vikao vinavyohudhuriwa na Mashia na Masunni ili kuendeleza zaidi umoja kati ya Waislamu.

Iran imetuma wasomaji Qur'ani Tukufu ambao wako katika kundi linalojulikana kama "Msafara wa Nur" kwenda Makka na Madina wakati wa msimu wa Hija mwaka huu wa 1444 Hijria kwa ajili ya kuandaa vikao vya Qur'ani na kusoma aya za Qur'ani Tukufu kwa ajili ya mahujaji kutoka kote duniani.

Mwaka huu, wasomaji na wahifadhi 20 wa Qur'ani kutoka mikoa 12 walijiunga na Msafara wa Nur ambao unaongozwa na Qari Maarufu Ustadh Ahmad Abolqasemi. Wameafiri hadi katika ardhi tukufu ya wahyi ikiwa ni katika fremu ya jitihada Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kueneza umoja mapenzi ya Qur'ani miongoni mwa Mahujaji.

Mahujaji wote wakiwemo wa madhehebu za Kiislamu za Shia na Sunni, walionyesha kuvutiwa sana na vikao vya Qur'ani vya Msafara wa Nur.

Hapa ni baadhi ya klipu za visomo vya Omid Hosseini-Nejad na Mohammad Mahdi Rouhani, wajumbe wawili wa msafara huo, wakati wa duru zilizohudhuriwa na Mahujaji mjini Makka.

 
 

Msafara huo unaundwa na Mohammad Hossein Saeidian, Omid Hosseini-Nejad, Mohsen Yar-Ahmadi, Ali Akbar Kazemi, Mohammad Ismail Khorshidi, Mohammad Kazemi, Seyed Mohammad Hosseinipour, Alireza Ateeqzadeh Rasul Tamjid, Mohammad Movahedian Attar, Ali Gholami, Ali Kabiri, Mohammad Mahdi Rouhani, na Mohammad Reza Jahdinia. Aidha kuna kunli la qasida linalojulikana kama Miad Tawasheeh linalojumuisha Baqer Savari, Ali Savari, Yaser Savari, Mansour Alavimaram and Ayub Tamimi. Msafara wa Nur wa Iran uliwasilia Saudi Arabia mapema Juni.

Wasomaji bora wa Qur'ani Tukufu  na vikundi vya qasida kutoka Iran hutumwa Saudi Arabia wakati wa Hijja kila mwaka kutekeleza programu za Qur'ani katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.

3483886

captcha