IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah

Matukio ya Jengo la Congress ni mfano halisi na wa wazi wa ubeberu na uistikbari wa Marekani

9:56 - January 09, 2021
Habari ID: 3473538
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema matukio ya hivi karibuni katika Bunge la Congress nchini Marekani yamepelekea Wamarekani wafahamu hatari ya rais wa nchi hiyo anayeondoka Donald Trump.

Aidha amesema matukio hayo ni mfano halisi na wa wazi wa ubeberu na uistikbari wa Marekani. Akizungumza Ijumaa usiku, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amesema yaliyojiri katika Bunge la Congress nchini Marekani ni muhimu. Amesema  tukio hilo ni sawa na ambalo Marekani imekuwa ikijaribu kuliibua nchini Lebanon kwa mwaka moja na nusu sasa.

Nasrallah ameongeza kuwa, Marekani imezoea kueneza yaliyojiri Congress katika nchi zingine ili kupindua serikali zingine duniani.

Trump alikuwa ni mfano wa wazi kabisa wa uistikbari na kiburi cha Marekani katika nyuga za kisiasa na kijeshi, amesema Nasrallah.

Kiongozi wa Hizbullah amekosoa vikali vitendo vya Marekani katika miaka ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na mauaji ya makamanda wa harakati za muqawama na mapambano ya Kiislamu hasa mashahidi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis.

Machafuko, fujo, vurugu, uporaji, ufyatuaji risasi, mauaji, ugaidi, mapinduzi, kukabiliana na mapinduzi; bali kwa kifupi; kashfa ya taifa, ndiyo maneno ambayo kila moja linafasiri matukio ya aibu yaliyotokea jana Jumatano, Januari 6, 2021 nchini Marekani ndani jengo la Congress

Matukio yote hayo yalitarajiwa kwani mambo yaliyojiri hivi karibuni ya kisiasa nchini Marekani, kuanzia uchaguzi mdogo wa maseneta wawili wa Georgia hadi kikao cha Congress cha jana Jumatano tarehe 6 Januari 2021 cha kupasisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais wa Novemba 3, 2020 yamezidi kuonesha mvurugano uliopo baina ya wanachama wa vyama viliwi vikuu vya Marekani vya Democratic na Republican.

3473639

captcha