IQNA

Watu wanne wauawa Marekani baada ya Trump kuchochea uvamizi wa Bunge la Congress, Biden ashinda +PICHA

11:40 - January 07, 2021
Habari ID: 3473532
TEHRAN (IQNA) - Watu wasiopungua wanne wameuawa baada ya waandamanaji wenye vurugu kuvamia Bunge la Marekani, Congress, mjini Washington DC wakitaka matokeo ya uchaguzi wa rais wa Novemba 3 yaliompa ushindi Joe Biden yabatilishwe.

Uvamizi huo wa Jumatano ulichochewa wazi wazi na rais Donald Trump anayeondoka na kupelekea kusitishwa kikao cha bunge ambacho kilikuwa kinapanga kuidhinisha ushindi wa Biden.

Kawaida vikao kama hivyo huwa vinachukua muda mfupi sana na vyenye kufurahiwa lakini wabunge wa Republican wamekuwa wakipinga baadhi ya matokeo ya uchaguzi.

Wafuasi wa Trump waliokuwa na hasira waliandamana huku wakiimba, "Tunamtaka Trump" huku mmoja wao akipigwa picha akiwa ameketi kwenye kiti cha rais wa bunge la Seneti.

Polisi Washington imesema kuwa ni wazi waandamanji hao walikuwa tayari kutumia nguvu yoyote ile kuingia katika majengo ya bunge.

Baada ya uvamizi huo uliochukua saa kadhaa, afisa anayesimamia mipangilio ya bungeni alitangaza kuwa sasa jengo hilo limenusuriwa na vikosi vya usalama.

Biden  amesema maandamano hayo "yamesababishwa na uchochezi na ni lazima hilo likome sasa", amesema.

Viongozi wengine wa kisiasa Marekani wamekosoa ghasia hizo huku kiongozi wa upinzani Sir Keir Starmer akitaja kitendo hicho kama "uvamizi wa moja kwa moja wa demokrasia".

Ghasia hizo ambazo wabunge wengi wa Marekani wamezitaja kuwa ni uhaini pia zimelaaniwa kimataifa. Waziri mkuu wa Uingereza Borris Johnson katika ujumbe wa twitter alielezea matukio katika bunge la Congress kama fedheha, akisema Marekani ilisimamia demokrasia kote duniani na kwamba ilikuwa muhimu kwamba kunakuwa na mabadiliko ya amani ya uatwala.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas alisema maadui wa demokrasia watatiwa hamasa na matukio ya vurugu katika eneo la Capitol, na kumtolea wito Trump kukubaliana na uamuzi wa raia.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel amesema kuwa aliamini sana Marekani "katika kuhakikisha ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani" kwa Bwana Biden, na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema ana matarajio makubwa ya ushirikiano na chama cha Democrat.

Biden atangazwa kuwa rais

Bunge la Congress la Marekani limemuidhinisha rasmi Joe Biden kuwa rais wa 46 wa nchi hiyo katika shughuli ambayo ilisitishwa kwa masaa kadhaa baada ya wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia bunge hilo na kupelekea watu wanne kuuawa.

Bunge la Congress limeidhinisha kura za wajumbe wa kamati maalumu ya uchaguzi nchini Marekani maarufu Electoral College. Biden alishinda kura 306 za wajumbe wa jopo maalumu Electoral College dhidi ya Trump aliyepata kura 232. 

Bunge la Congress la Marekani limemuidhinisha rasmi Joe Biden kuwa rais wa 46 wa nchi hiyo katika shughuli ambayo ilisitishwa kwa masaa kadhaa baada ya wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia bunge hilo na kupelekea watu wanne kuuawa.

Bunge la Congress limeidhinisha kura za wajumbe wa kamati maalumu ya uchaguzi nchini Marekani maarufu Electoral College. Biden alishinda kura 306 za wajumbe wa jopo maalumu Electoral College dhidi ya Trump aliyepata kura 270. 

UN yataka wanasiasa waheshimu uamuzi wa wananchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na yaliyojiri Jumatano mjini Washington DC nchini Marekani na kuwataka viongozi wa kisiasa kuwaasa wafuasi wao kujizuia na ghasia.

una wasiwasi mkubwa kuwa  baada ya Bunge la Congress kumuidhinisha Biden kuwa rais wa Marekani, wafuasi wa Trump watendeleza maandamano na ghasia kote katika nchi hiyo ambayo sasa imegawanyika katika kambi mbili hasimu.

3946245

Kishikizo: marekani trump biden bunge
captcha