IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kuingizwa chanjo ya Marekani na Uingereza nchini Iran ni marufuku, hawaaminiki

16:42 - January 08, 2021
Habari ID: 3473535
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametangaza bayana kuwa, kuingizwa Iran chanjo ya corona au COVID-19 kutoka Marekani na Uingereza ni marufuku.

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo Ijumaa kwa mnasaba wa maadhimisho ya mapambano ya Dei 19 ya wananchi wa Qum dhidi ya utawala wa kiimla uliopinduliwa wa Shah.

Katika sehemu ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei ametangaza bayana kuwa, kuingizwa chanjo ya COVID-19 kutoka Marekani na Uingereza nchini Iran ni marufuku na kuongeza kuwa: “Tayari nimeshawafahamisha maafisa wa serikali, na sasa natangaza hadharani kuwa, uagizwaji wa chanjo za Marekani na Uingereza ni marufuku.”

Ameongeza kuwa, “Kama Wamarekani wengeweza kuzalisha chanjo basi hawangekumbwa na fedheha hii ya corona katika nchi yao ambapo karibu watu elfu nne wanapoteza maisha kila siku. Aidha kimsingi hatuwaamini kwa sababu baadhi ya chanjo hizo hutumika kama mbinu ya majaribio kwa mataifa mengine."

Kiongozi Muadhamu amekumbusha kashfa ya muongo wa 90  ambapo Ufaransa ilituma Iran damu ambayo ilikuwa imewekwa virusi vya ukimwi.

Ayatullah Khamenei amesema serikali ya Iran inaruhusiwa kununua chanjo ya corona kutoka nchi zingine zenye kuaminika. Aidha amepongeza chanjo ya corona  iliyotengenezwa Iran na kuitaja kuwa chanzo cha fahari na heshima.

Kurejea Marekani katika JCPOA bila vikwazo kuondolewa ni kwa madhara yetu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, uamuzi wa bunge na serikali ya Iran kupunguza utekelezwaji wa baadhi ya ahadi za nchi hii katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni uamuzi sahihi na wa kimantiki kabisa na kuongeza kuwa: "Kuna uwezekano wa Marekani kurejea katika JCPOA bila vikwazo kuondolewa na hilo likifanyika litakuwa kwa madhara yetu."

Katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu ameashiria kuanza urutubishaji wa asilimia 20 wa madini ya urani nchini Iran na kuongeza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haisisitizi na wala haina haraka ya kuona Marekani inarejea katika JCPOA bali mantiki yetu ni kuondolewa vikwazo na kurejeshewa haki  ambazo taifa limepokonywa na hilo ni jukumu la Marekani na Ulaya."

Kiongozi Muadhamu amesema iwapo vikwazo vitaondolewa basi kurejea Marekani katika JCPOA kutakuwa na maana. Aidha amesema nukta itakayofuata baada ya hapo ni Iran kulipwa fidia kutokana na hasara ilizopata. 

Fedheha katika uchaguzi wa Marekani

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mvurugiko wa sanamu kubwa la uistikbari (yaani Marekani) na kusema: " 'Fedheha katika uchaguzi' na 'haki za binadamu ambazo hupelekea mtu mweusi kuuawa mara kwa mara na watenda jinai hiyo kutochukuliwa hatua,' ni mambo ambayo yameweka wazi utambulisho wa thamani za Marekani ambazo sasa zinadhihakiwa duniani kote hata  miongoni mwa marafiki wa Marekani." Kiongozi Muadhamu amesema uchumi wa Marekani umelemaa na kuongeza kuwa, kuwepo makumi ya mamilioni ya watu wasio na ajira, wenye njaa na wasio na nyumba ni ishara ya hali mbaya nchini Marekani. Amesema hilo si jambo la kushangaza lakini la kushangaza ni kuwa kuna wale ambao bado tumaini lao kuu liko Marekani.

Uwezo wa Iran

Ayatullah Khamenei aidha amesema maana na mantiki ya Iran kuwepo katika eneo ni kuwapa nguvu marafiki na waungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa: "Uwepo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo unaleta uthabiti na unapelekea kuondoa ukosefu wa uthabiti kama ilivyoshuhudiwa huko Syria na Iraq na huu ni ukweli ambao wote wanaufahamu; kwa msingio huo uwepo huu ni wa hakika na unapaswa kuwepo na utaendelea kuwepo."

Kiongozi Muadhamu amekumbusha kuhusu uwezo mkubwa wa kujihami wa Iran hii leo na kutoa mfano wa kutunguliwa ndege vamizi ya Marekani katika anga ya Iran au kushambuliwa kituo cha kijeshi cha Marekani cha  Ain al-Assad na kusema: "Katika kukabiliana na ukweli huu, adui hana budi ili kuzingatia uwezo wa kujihami wa Iran katika mahesabu na maamuzi yake."

3946372

captcha