IQNA

Al Azhar

Mwanachuoni wa Al-Azhar asema Tafsiri Mpya za Qur’ani zinahitajika

21:26 - January 21, 2024
Habari ID: 3478228
IQNA - Msomi na afisa wa zamani wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri amesisitiza ulazima

"Tunakabiliwa na shida katika kuelewa malengo ya Qur'ani na sayansi ya Qur'ani," Hamd Salim Abu Asi alisema katika mahojiano ya televisheni.

Alisema tafsiri za Qur'ani zilizopo leo aghalabu husimulia na kuchambua yale ambayo yamesemwa huko nyuma, tovuti ya ad-Dustur iliripoti.

Wafasiri wa Quran katika siku za nyuma waliandika ufafanuzi wao kwa kuzingatia utamaduni wa wakati wao, alibainisha.

"Leo, tunahitaji tafsiri za kisasa za Qur’ani Tukufu na vile vile Fiqh ya kisasa (sheria ya Kiislamu) ili tuweze kulinda misingi  isiyobadilika na kukubali mabadiliko na mapitio (kwa maoni ya zamani)."

"Tunahitaji tafsiri inayoonyesha utu wa binadamu na kukubali maoni na mitazamo ya wengine," alisisitiza.

Mwenyezi Mungu ameituma dini kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu na hukumu zake nyingi zinaweza kubadilika mara kwa mara au mahali tofauti, Abu Asi aliongeza.

Kwingineko katika matamshi yake, alitahadharisha kuhusu kujipenyeza kwa Masalafi au Mawahhabi katika Chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar na akasema hatari ya ugaidi wa kiakili (unaosababishwa na Masalafi) ni sawa na ugaidi wa kutumia silaha.

Al-Azhar ni msikiti wa kihistoria, kituo cha Kiislamu na chuo kikuu cha Kiislamu huko Cairo, mji mkuu wa Misri.

Khalifa wa zama za  Fatimiyya aliagiza ujenzi wake kwa jiji kuu jipya lililoanzishwa mwaka wa 970 Miladia.

3486884

captcha