IQNA

Mazungumzo baina ya dini

Al-Azhar yahimiza mkutano wa kimataifa kujibu maswali kuhusu Qur'ani

19:32 - July 16, 2023
Habari ID: 3477293
CAIRO (IQNA) - Sekretarieti ya Baraza la Wanazuoni la Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri imetoa wito wa kufanyika kongamano la kimataifa ili kujibu maswali kuhusu Qur'ani Tukufu.

Baraza hilo limetoa tamko hilo katika kongamano lake la 19 la wasomi mapema wiki hii, tovuti ya Al-Luwa iliripoti.

Kongamano hilo ambalo lilifanyika  kwa uungaji mkono wa Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Sheikh Ahmed al-Tayeb, ilihudhuriwa na katibu wa baraza Sheikh Hassan al-Saghir, Tafsir na mtaalamu wa sayansi ya Qur'ani Tukufu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar Arafat Othman, na mjumbe wa Majlisi ya Mafunzo ya Kiislamu Mahmoud Othman, miongoni mwa wengine.

Sheikh al-Saghir alisema katika hotuba yake kwenye mkutano huo kwamba Qur'an ndiyo chimbuko la kanuni za Sharia, itikadi na maadili ya Kiislamu na sio kitabu tu cha kusoma kwa ajili ya baraka.

Aliongeza kuwa Qur'ani Tukufu ni sheria inayogusia nyanja zote za maisha ya Waislamu.

Mahmoud Othman pia ameashiria hadhi ya Qur'ani Tukufu na akasema kongamano la kimataifa kwa ajili ya kujibu maswali na shaka kuhusu mafundisho na amri za Kitabu hicho Kitukufu.

Ameongeza kuwa kufasiri Qur'ani Tukufu na kutoa hukumu kutokana na mafundisho yake kunahitaji maarifa maalum katika nyanja tofauti.

Si kila mtu ambaye ana elimu ndogo kuhusu sayansi ya Kiislamu anayeweza kudai kuwa na uwezo wa kutoa hukumu kwa mujibu wa Qur'ani na kuhusisha hukumu hiyo na Kitabu Kitukufu, aliongeza.

3484348

Kishikizo: al azhar qurani tukufu
captcha