IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Nchi 12 zashiriki Mashindano ya Qur'ani ya Kituo cha Dar ul Qur’an ya Imam Ali

22:41 - December 16, 2023
Habari ID: 3478045
IQNA - Wahifadhi na wasomaji Qur'ani kutoka nchi 12 walishiriki katika toleo la mwaka huu la mashindano ya Qur'ani yaliyoandaliwa na Kituo cha Dar-ul-Quran cha Imam Ali (AS) nchini Iran.

Mohammad Ansari, mkuu wa kituo hicho, alisema kuwa washiriki 362 wanatoka nchi za nje, zikiwemo Afghanistan, Pakistan, Tajikistan, Iraq, Jamhuri ya Azerbaijan, India, Nigeria, Lebanon, Tanzania, Ukraine, Uhispania na Syria.

Aliyasema hayo Ijumaa katika hafla ya kuhitimisha toleo la 17 la mashindano hayo, iliyofanyika kwenye haram ya Hadhrat Abdul Azim Hassani (AS) huko Rey, kusini mwa Tehran.

Alisema wanaharakati 9,000 wa Qur'ani walishiriki katika toleo hili, wakishindana katika kategoria tofauti kama vile usomaji wa Qur'ani, kuhifadhi (viwango tofauti), Tarteel, na dhana za Qur'ani.

Jumla ya wataalamu 72 wa Qur'ani walitathmini maonyesho ya washiriki katika kategoria mbalimbali, afisa huyo alisema.

Pia alibainisha kuwa waandaaji wanapanga kuanzisha mabadiliko mapya kwenye shindano hilo, ambayo yatatekelezwa katika toleo la mwaka ujao.

Idadi kadhaa ya shakhsia  na wanaharakati wa Qur'ani Tukufu walihudhuria hafla ya kutunuku tuzo hizo jana.

12 Countries Attend Imam Ali Dar-ol-Quran Center’s Quran Contest  

Wanaharakati wawili wakongwe wa Qur’ani Tukufu, Ahmad Hajisharif na Zahra Sarihinejad walitunukiwa katika hafla hiyo kwa huduma zao za Qur’ani Tukufu.

Kituo cha Dar ul Qur’an ya Imam Ali (AS) kila mwaka huandaa shindano hilo ili kukuza ujifunzaji wa Qur'ani na kutambua vipaji vya Qur'ani.

3486438

Habari zinazohusiana
captcha