IQNA

Harakati za Qur'ani

Wanafunzi 1,000 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kuhitimu katika chuo cha Dar-ul-Quran Gaza

19:01 - June 08, 2023
Habari ID: 3477117
Mkuu wa Kituo cha Dar-ul-Quran na Sunnah cha Gaza huko Palestina amesema zaidi ya wahifadhi 1,000 wa Qur'ani Tukufu wanatarajiwa kuhitimu kutoka kituo hicho mwishoni mwa majira ya kiangazi.

Bilal Imad alisema pamoja na kuanza kwa sikukuu za majira ya joto, shughuli za kuhifadhi Qur'ani Tukufu zimeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kituo hicho na wale wanaojifunza Qur'ani Tukufu kwa moyo wameongeza juhudi kwa kuwa wana muda mwingi wa kuhifadhi.
Alibainisha kuwa baadhi ya wanafunzi sasa wana mara mbili ya muda waliokuwa nao hapo awali wa kuhifadhi Qur'ani, tovuti ya habari ya al-Risalah iliripoti.
Mipango inaendelea kusaidia wanafunzi kutumia vyema wakati wao wa ziada katika majira ya joto, Imad alisema.
Amewataka wananchi wa Ukanda wa Gaza kuchangamkia fursa hiyo na kuwapeleka watoto wao katika vituo vya Qur'ani wakati wa likizo za kiangazi.
Vile vile amebainisha kuwa pamoja na kuhifadhi, Dar-ul-Quran na Sunnah imeanzisha kozi za Qur'ani katika nyuga za kisomo na Lahn.
Pia kuna kozi za mtandaoni za Qur'ani zinazoandaliwa na kituo hicho kwa kushirikisha wanafunzi kutoka nchi nyingine, aliendelea kusema.
Licha ya mzingiro wa miaka mingi wa Ukanda wa Gaza na vita kadhaa vilivyowekwa kwenye eneo la pwani na utawala wa Kizayuni, shughuli za Qur'ani zikiwemo kozi za Qur'ani, mashindano na programu nyinginezo ni za kawaida sana huko.
 
4146389

captcha