IQNA

Jinai za Israel

Nchi za Kiarabu, Kiislamu zalaani hujuma ya Israel dhidi ya Wapalestina ndani ya Msikiti wa Al Aqsa

12:12 - April 06, 2023
Habari ID: 3476819
JTEHRAN (IQNA)- umuiya ya Nchi za Kiarabu imelaani vikali hujuma ya hivi karibuni zaidi ya utawala haramu Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa katika Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel. Jumuiya hiyo pia limelaani hujuma ya kikatili ya askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa katika msikiti huo kwa ajili ya ibada katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Nchi za Kiarabu zaitisha kikao cha dharura kulaani uvamizi wa Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imelaani vikali hujuma ya hivi karibuni zaidi ya utawala haramu Israel dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa katika Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel. Jumuiya hiyo pia limelaani hujuma ya kikatili ya askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa katika msikiti huo kwa ajili ya ibada katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Jumuiya hiyo yenye wanachama 22 ilifanya mkutano wa dharura siku ya Jumatano ili kujadili uvamizi wa hivi punde wa eneo hilo takatifu la Waislamu uliofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel .

Baraza la Mawaziri la Umoja wa Kiarabu lilisema katika taarifa yake kwamba, "Tunalaani vikali uhalifu wa wavamizi dhidi ya waumini wasio na ulinzi katika Msikiti wa al-Aqsa,"

Aidha taarifa hiyo imesema, "Tunalaani vikali ukiukaji na mashambulizi yoyote yanayofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo."

Jumuiya hiyo imesisitiza kuhusu haki ya Waislamu na Wakristo kufika kwa njia salama na isiyo vikwazo kwenye maeneo yao ya ibada na kuhubiri kwa uhuru na kutekeleza imani zao za kidini katika mji wa Quds.

Baraza hilo limezitaka nchi wanachama kuchukua hatua zinazohitajika katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na kuanzisha hatua kali ya kidiplomasia, kwa ajili ya kuulinda mji wa Quds, kutetea matukufu yake ya Kiislamu na Kikristo, na kuunga mkono kisiasa, kijamii. kiuchumi na haki za binadamu za wakazi wa mji huo.

Kwingineko, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hujuma na shambulio la kinyama la vikosi vya utawala ghasibu vya Kizayuni dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa katika ibada ya itikafu katika msikiti wa Al-Aqswa kwa mara nyingine imeweka bayana sura ya kinyama na kikatili ya utawala huo na ukiukaji wa haki za binadamu.

Nasser Kanaani ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijami wa twitter kwamba: Tunalaani vikali jinai iliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.

Askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Jumanne walivamia Msikiti wa Al-Aqsa na kuwatia nguvuni Wapalestina kadhaa waliokuwa kwenye itikafu na ibada zingine za mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hii si mara ya kwanza katika mwezi huu mtukufu wa kwa jeshi la Israel kuvamia na kuwatia mbaroni waumini katika msikiti wa al-Aqswa.

4131855

captcha