IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Kizayuni wauhujumu msikiti wa al-Aqswa chini ya himya ya jeshi katili la Israel

19:24 - June 08, 2023
Habari ID: 3477120
Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali asubuhi ya leo wameuvamia tena msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kulivunjia heshima eneo hilo takatifu.

Ripoti zinaeleza kuwa, makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurut ada wamevamia msikiti wa al-Aswa na kufanya vitendo vya kichochezi.

Mashuhuda wanasema kuwa, uvamizi wa walowezi hao wenye itikadi kali ulifanyika chini ya ulinzi mkali kutoka kwa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel ambao walikuwa wakiwalinda walowezi hao.

Katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno sambamba na njama za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa eneo hilo takatifu.

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kuyazayunisha maeneo hayo na kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

Hali Ukanda wa Gaza

Wakati huo huo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Maji ya Ghaza ameeleza kuwa: Asilimia 97 ya maji katika nyumba za raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza hayanyweki.

Munzir Salim Mkurugenzi wa Taasisi ya Maji ya Ukanda wa Ghaza amesema kuwa asilimia 97 ya maji katika nyumba za Wapalestina wakazi wa Ukanda wa Ghaza hayanyweki na kutahadharisha juu ya madhara yanayoweza kusababishwa na maji hayo kwa Wapalestina zaidi ya miloni mbili wa eneo hilo.  

Munzir Salim ameongeza kuwa, maji ya mabomba ya nyumba za Wapalestina katika Ukanda wa Gaza hayanyweki, na wanayatumia kwa shughuli nyingine za nyumbani. 

Amesema, hali hii tajwa ni kengele ya hatari inayoashiria ukosefu wa vyanzo vya maji salama kwa ajili ya raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza ikiwa ni pamoja na maji ya chini ya ardhi na vyanzo vingine mbadala.  

Mzingiro wa zaidi ya miaka 16 wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza  umekuwa na taathira hasi na kuzidisha matatizo kwa maisha ya raia wa Palestina zaidi ya milioni mbili wa eneo hilo. 

4146475

captcha