IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Kampeni ya kuusafisha Msikiti wa al-Aqsa kakbla ya mwezi wa Ramadhani

21:48 - March 19, 2023
Habari ID: 3476728
TEHRAN (IQNA)- Mamia ya Wapalestina wakazi wa mji wa Al Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel wameanzisha kampeni ya kuusafisha Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa sambamba na kukaribia mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Katika kampeni hiyo, mamia ya Wapalestina wanaojitolea na kushughulika na hafla za kitaifa na Kiislamu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu wanashiriki katika kazi ya kuunadhifisha msikiti wa Al Aqsa zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
Katika kampeni hiyo, wanashiriki vijana na wazee, wanawake na vijana chipukizi kutoka mji wa Al Quds au Baitul Muqaddas, ambapo miongoni mwa kazi wanazofanya ni pamoja na kusafisha msikiti wa Al-Aqsa, kuosha vioo na vigae, milango na sehemu za uwanja wa mahali hapo patakatifu.

Walowezi wa Kizayuni huwa wanauvamia na kuuvunjia heshima msikiti wa Al-Aqsa takribani kila siku, huku likiwa ni jambo la kawaida pia kwa askari wa utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel kuwafyatulia risasi na mabomu ya gesi Waislamu Wapalestina wanaokwenda kusali msikitini humo.

Inatarajiwa kuwa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, makumi ya maelfu ya watu watahudhuria katika msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu na moja ya maeneo matatu matakatifu baada ya Makka na Madina, kushiriki katika Sala na ibada zingine maalumu za mwezi huo mtukufu.
3482862
captcha