IQNA

Zilzala Uturuki na Syria

Sheikh al-Qaradaghi: Waislamu watumie fedha za Umrah kuwasaidia waathiriwa wa Zilzala

17:33 - February 14, 2023
Habari ID: 3476559
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) ametoa wito kwa Waislamu walionuia kutekeleza safari ya ibada ya Hija ndogo ya Umrah kusitisha safari hiyo kwa sasa na badala yake kutumia fedha hizo kuwasaidia wahanga wa mitetemeko (zilzala) ya ardhi Uturuki na Syria.

Sheikh Dr Ali Mohiuddin al-Qaradaghi, Katibu Mkuu wa IUMS hasa amewataka wale wanaotaka kutekeleza ibada ya Umra kwa niaba ya wengine au wale wamepanga kuelekea Umrah lakini wameshawahi tekeleza ibada hiyo mara kadhaa kusitisha safari kwa sasa na badala yake fedha hizo wazitumie kuwasaidia waathirika wa mitetemeko mikubw aya ardhi  Syria na Uturuki.

Matetemeko mawili makubwa ya ardhi yalitikisa maeneo ya kusini mwa Uturuki Jumatatu iliyopita, na kuua watu wasiopungua 37,000 katika nchi zote mbili na kuathiri mamilioni ya wengine.

Usaidizi huu, Al-Qaradaghi alidumisha, una thawab (thawabu) zaidi na kipaumbele kwani unaweza kupunguza uchungu na kuokoa maisha, Arabi21 iliripoti.

Kuokoa wahasiriwa ni jukumu la kidini kwa nchi za Kiislamu, alisema, akirejea aya ya 32 ya Surah al-Maidah inayosomeka "kuokoa maisha itakuwa ni fadhila kubwa kama kuokoa wanadamu wote."

Tetemeko la kwanza la  ardhi la ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha Rishta lilitikisa kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria Jumatatu asubuhi ya tarehe 6 Februari. Kitovu chake kilikuwa ni katika mji wa Gaziantep wa Uturuki ambapo mamia ya majengo yameporomoka.Masaa machache baadaye kulijiri mtetemeko mwingine wa ardhi uliokuwa na ukubwa 7.6 kwenye kipimo cha rishta. Baada ya hapo pia kumejiri idadi kubwa ya mitetemeko midogo.

Hadi sasa watu wasiopungua 37,000 wamepoteza maisha kutokana na mitetemeko hiyo weng wakiwa nchni Uturuki.

Umoja wa Mataifa unakadiria hadi watu milioni 5.3 nchini Syria wanaweza kukosa makazi baada ya mitetemeko hiyo ardhi. Takriban watu 900,000 wanahitaji chakula cha moto haraka nchini Uturuki na Syria.

Sheikh al-Qaradaghi ameendelea kusema kuwa, misaada kwa waathirika katika nchi hizo mbili ina thawabu zaidi na ni kipaumbele kwani inaweza kupunguza uchungu na kuokoa maisha.

Kuokoa wahasiriwa ni jukumu la kidini kwa nchi za Kiislamu, alisema, akiashiria aya ya 32 ya Surah al-Maidah inayosema "…Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote…"

Umoja wa Mataifa unakadiria hadi watu milioni 5.3 nchini Syria wanaweza kukosa makazi baada ya tetemeko la ardhi. Takriban watu 900,000 wanahitaji chakula cha moto haraka nchini Uturuki na Syria.

3482467

captcha