IQNA

Matukio ya Palestina

Chuo Kikuu cha Kiislamu cha kimatiafa kujengwa Istanbul

19:17 - June 08, 2023
Habari ID: 3477119
Chuo kikuu jumuishi cha kimataifa cha mafundisho ya Kiislamu kimepangwa kuanzishwa mjini Istanbul, Uturuki.

Mehmet Gormez, mkuu wa zamani wa Urais wa Uturuki wa Masuala ya Kidini (Diyanet) alisema hayo katika mkutano nchini Qatar na Sheikh Ali al-Qaradaghi, katibu mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS).

Ameongeza kuwa kituo hicho cha kitaaluma kitaanzishwa kwa kuzingatia kanuni na maadili ya Kiislamu, tovuti ya IUMS iliripoti.

Gormez alisema wakati Mehmed II, anayejulikana kama Mehmed Mshindi, alipoiteka Istanbul katika karne ya 15, aliwaalika wanazuoni wa Kiislamu kwenye mji huo na sasa Istanbul itarejea tena kuwa kituo cha mkusanyiko wa wasomi wa Kiislamu

Wakati wa mkutano huo,  Sheikh al-Qaradaghi na Gormez, ambaye anazuru Qatar kwa mwaliko wa Kitivo cha Mafundisho ya Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Hamad Bin Khalifa (HBKU), walijadili masuala kama vile uchaguzi wa hivi karibuni wa rais na bunge nchini Uturuki.

Wakati akiwa Doha, Gormez pia alitoa hotuba katika HBKU kuhusu wasomi wa Kiislamu wa siku zijazo.

 

4146170

captcha