IQNA

Jeshi katili la Israel lamuua shahidi kijana Mpalestina

20:36 - September 05, 2022
Habari ID: 3475735
TEHRAN (IQNA)- Vikosi vya kijeshi vya utawala ghasibu wa Israel vimempiga risasi na kumuua shahidi kijana mwingine wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo siku ya Jumatatu.

Mpalestina huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 alipigwa risasi na kuuawa na jeshi la Israel wakati wa uvamizi mapema Jumatatu huko Qabatiya, kusini mwa Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu, Wizara ya Afya ya Palestina imesema.

"Taher Mohamed Zakarneh aliuawa kwa kupigwa risasi na wavamizi (wa Israeli) huko Qabatiya," taarifa ya wizara imesema.

Alipoteza maisha baada ya "kulazwa hospitalini akiwa na majeraha ya risasi kichwani, kwenye mguu wa kulia, kwenye paja la mguu wa kushoto na kuchomwa moto", taarifa hiyo imeongeza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imelaani mauaji hayo na kuyataja kuwa ya kiholela. Kijana mwingine alijeruhiwa na wengine watatu kuzuiliwa mjini Qabatiya, kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina Wafa.

Hayo yanajiri wakait ambao hivi karibuni  Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Palestina, limesema "Hadi kufikia sasa mwaka huu, mashambulizi ya Jeshi la Utawala wa Israel yamewaua Wapalestina 111, watoto 24 na wanawake 8."

Aidha taarifa hiyo imebaini kuwa, takriban Wapalestina 1,277 walijeruhiwa, wakiwemo watoto 195, wanawake 39 na waandishi wa habari 22, huku Wapalestina watatu, akiwemo mwanamke mmoja, wakifariki dunia katika magereza ya Israel katika kipindi hicho.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Palestina limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jina, ICC, kuchukua hatua kwa umakini kuhusiana na hali ya Palestina sawa na hatua yake ya haraka nchini Ukraine.

3480350

 

3480350

captcha