Mahafali ya kuhitimu wanafunzi hao 700 imefanyika katika jimbo la Oromia katika Kituo cha Kiislamu cha Zayd Bin Thabit.
Mhubiri maarufu wa Ethiopia, Sheikjh Amin Ibro ameseambaza picha na klipu za mahafali hiyo ambapo wanafunzi wanafunzi wanaonekana wakiwa wanashiriki katika sherehe za kuhitimu kwao.
Waislamu ni karibu asilimia 35 ya watu wote milioni 110 nchini Ethiopia wakiafuatiwa na Wakristo wa Kiorthodoxi ambao ni takribani asilimia 40.