IQNA

Njama za utawala wa Kizayuni za Kuuyahudisha Msikiti wa Al Aqsa

19:48 - December 31, 2021
Habari ID: 3474749
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza njama zake haramu za Kuuyahudisha Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.

Ofisi ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Msikiti wa Al-Aqsa imetangaza kuwa, walowezi zaidi ya 34,000 wa Kizayuni wamefanya mashambulizi dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa mwaka huu unaomalizika leo wa 2021.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Msikiti wa Al-Aqsa Sheikh Azzam Al-Khatib amesema kuwa: "Zaidi ya walowezi 34,112 wa Kizayuni wameushambulia Msikiti wa Al-Aqsa mwaka huu (2021)."

Al-Khatib amesisitiza kuwa, mashambulizi ya walowezi hao dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa yanatekelezwa kwa uungaji mkono na himaya ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umeugeuza msikiti huo kuwa kambi ya kijeshi.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Msikiti wa Al-Aqsa pia ametahadharisha kuhusu kuongezeka mashambulizi ya Mayahudi wenye misimamo mikali dhidi ya Msikiti wa Al-Aqswa na kuuvuinjia heshima msikiti huo mtukufu.

Msikiti wa Al-Aqsa, ambaoni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Palestina katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem), daima umekuwa ukilengwa wa hujuma na vitendo vya uharibifu vya utawala ghasibu wa Israel na walowezi wa Kizayuni. 

Kwingineko, Mpalestinaq ameuawa shahidi Jumatano wakati makumi ya walowezi wa Kizayuni wamefanya hujuma na mashambulio dhidi ya nyumba za Wapalestina katika kitongoji cha al-Laban kusini mwa mji wa Nablos kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Katika hujuma hiyo, walowezi hao wabaguzi wa Kizayuni wameharibu mali na milki za Wapalestina wa eneo hilo.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hivi karibuni, mabuldoza ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel yalivamia maeneo ya kaskazini mwa mji wa Quds na kuharibu mali na miliki za Wapalestina katika maeneo hayo.

Wanajeshi wa Israel wakiongozwa na mabuldoza walivamia kitongoji kimoja jirani na kivuko cha Qalandiya kaskazini mwa Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuharibu mali na miliki kadhaa za Wapalestina.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema katika ripoti yake kwamba, vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na Israel vimeshadidi mno tangu kuanza mwaka huu wa 2021.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mwaka uliopita wa 2020 utawala wa Kizayuni wa Israel ulibomoa nyumba karibu 689 katika Ukingo wa Magharibi na Quds tukufu na kulazimisha mamia ya familia za Wapalestina kuwa wakimbizi. 

4024946

captcha