Zawadi hizo zimetunukiwa hospitali hiyo kwa mnasaba wa siku ya kukumbuka kuzaliwa Imam Ali AS, Imamu wa Kwanza wa Waislamu wa Kishia na Khalifa wa Nne.
Misaada ya hivyo iliyojumuisha vyakula na bidhaa za kiafya imekabidhiwa wakuu wa hospitali hiyo na Sheikh Suleiman Nadi Bamba, ambaye ni Imamu wa kituo hicho. Amesema kitendo chao ni mfano wa alivyokuwa Imam Ali AS.
Sheikh Bamba amesema Kituo cha Kiislamu cha Imam Baqir AS kitaendelea kusaidia jamii ya Ghana kiuchumi na kijamii ili kuondoa matatizo ya kimaisha.
Aidha amesema ni jukumu la kila Muislamu kusaidia jamii ya mwanadamu katika zama hizi za janga la COVID-19.