IQNA

Mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana

Jerry Rawlings aliiga nadharia za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

22:04 - November 24, 2020
Habari ID: 3473388
TEHRAN (IQNA) – Jerry Rawlings, Rais wa zamani wa Ghana ambaye amefariki hivi karibuni akiwa na umri wa miaka 73, alikuwa mwanasiasa Mkristo ambaye aliathiriwa na kuiga baadhi ya fikra za Mapinduzi ya Kiislamu.

Hayo yamedokezwa na Bw.  Muhsin Muarifi Mkuu wa Idara ya Utafiti wa Ukanda wa Nchi za Kiarabu na Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa Al Mustafa SAW, ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana, ametaja hayati Rwalings kuwa ni shujaa wa kitaifa Ghana.

Katika mahojiano maalumu na IQNA, ameongeza kwamba Rawlings alikuwa muungaji mkono wa watu waliotengwa  na waliodhulimiwa Ghana na pia kote katika bara la Afrika.

Rawlings, aliyeingia madarakani kufuatia mapinduzi mawili ya kijeshi kabla ya kuanzisha utawala wa kidemokrasia nchini mwake, alifariki dunia tarehe 12 mwezi huu wa Novemba akiwa na umri wa miaka 73.

Uhusiano mzuri wa Iran  na Ghana

Ameongeza kuwa, uhusiano mzuri ulioko baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Ghana hivi sasa ni kati ya turathi zenye thamani za Rawlings. Baadhi ya waandishi wa Ghana katika kumbukumbu zao wameandika kuwa mapinduzi yaliyomleta Rawlings madarakani kwa kiasi fulani yaliiga baadhi ya nadharia za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Kutetea hakia na uadilifu, kuwasaidia watu waliotengwa na kudhulumiwa katika jamii na kupambana na mabeberu na wakoloni ni nukta za pamoja ambazo zimeyakurubisha mataifa ya Iran na Ghana, amesema Bw. Muarifi.

Misaada ya Iran kwa Ghana

Shahidi Sayyid Hassan Shahcheraghi, ambaye alikuwa mwakilishi wa jimbo la Damghan katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika muongo wa 80 alitembelea Ghana wakati wa urais wa Rawlings na alinukuliwa akisema: “Katika kikao na wakuu wa Ghana, walisema wanafuatilia kwa karibu matukio ya Iran.” Taasisi ya Jihadi ya Ujenzi Mpya ya Iran ilishiriki katika miradi mbali mbali ya maendeleo Ghana wakati wa urais wa Rwalings ikiwa ni pamoja kuwajengia wasiojiweza nyumba na pia kujenga misikiti na shule zaidi ya 200 katika eneo la kaskazini mwa Ghana. Aidha Iran inashiriki katika ustawi wa kilimo nchini Ghana.

Rawlings alitetea Iran

Katika vikao vya kimataifa Rawlings alitetea sana Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakati wa vita vya kulazimishwa vya utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya Iran.

Bw. Muarifi anasema Rawlings aliwahi kutembelea Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana ambapo aliyapongeza sana Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

 

//«جری راولینگز»؛ سیاستمدار مسیحی متأثر از انقلاب در غنا بود/ سکانداری پیشرفت سیاسی و اقتصادی در قاره سیاه

Wa kwanza upande wa kulia ni Bw. Muhsin Muarifi akiwa na Jerry Rawlings (wa tatu kutoka kulia) katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana

Jerry Rawlings, wakati huo akiwa Luteni katika kikosi cha jeshi la wanaanga, alimpindua Jenerali Frederick Akuffo mnamo mwaka 1979 na kuongoza nchi ya Ghana kwa kipindi kifupi na kisha kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia kabla ya kufanya mapinduzi mengine miaka miwili baadaye, akibaini kwamba serikali ilishindwa kukomesha ufisadi na hakukuwa na uongozi bora.

Kuanzia mwaka 1981 hadi 1993, Jerry Rawlings aliongoza serikali iliyoundwa na wanajeshi na raia. Mnamo 1992, alichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri chini ya katiba mpya na alichukua madaraka mwaka uliofuata kwa mihula miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa John Kufour mnamo mwaka 2001.

3936092

captcha