IQNA

Spika wa Bunge: Kuwait haitafunga misikiti tena

21:15 - February 08, 2021
Habari ID: 3473632
TEHRAN (IQNA) – Spika wa Bunge la Kuwait amesema nchi hiyo haina nia ya kufunga misikiti tena ili kuzuia kuenea kirusi cha corona au COVID-19.

Marzouq Ali Mohammed Al-Ghanim ameanduka ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter ambapo amekanusha uvumi kuhusu kufungwa misikiti nchini humo.

Amesisitiza kuwa misikiti haitafungwa lakini kutachukuliwa hatua za kuzuia maambukizi ya corona.

Awali kulikuwa na uvumi kuwa Kuwait itaanza kutekeleza sheria mpya za kuzuia corona kabla ya kuanda Mwezi Mtufuku wa Ramadhani ambapo sala za jamaa zitapigwa marufuku.

Hatua kadhaa za kuzuia kuenea corona zinaendelea kutekelezwa nchini kuwa.  Mwezi uliopita wa Disemba Kuwait ilizindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya corona.

Kuwait ilikuwa miongoni mwa nchi kadhaa za Kiarabu ambazo zilifunga misikiti kwa takribani miezi sita kuanzia mwezi mwachi mwaka 2010 ili kuzuia kuenea corona.

Hadi kufikia sasa watu takribani 171,000 wameambukizwa corona nchini Kuwait na miongoni mwaka 966 wamepoteza maisha.

3952682

Kishikizo: kuwait msikiti Corona
captcha