IQNA

Siasa

Matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Kuwait yaibua matumiani katika vita dhidi ya ufisadi

19:07 - June 08, 2023
Habari ID: 3477118
Mrengo wa upinzani nchini Kuwait kwa mara nyingine tena umeshinda wingi wa viti vya Bunge nchini humo katika uchaguzi mkuu wa saba wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi huku kukiwa na matumiani kuwa ushindi huo utafanikisha vita dhidi ya ufisadi nchini humo.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo, wabunge wa upinzani wamepata wingi wa viti katika Bunge la Kuwait katika uchaguzi mkuu wa saba wa nchi hiyo na hivyo kulidhibiti Bunge hilo. Bunge la Kuwait limevunjwa mara kadhaa tangu 1962.

Uchaguzi wa siku ya Jumanne ulifanyika baada ya Mahakama ya Katiba ya Kuwait mwezi Machi kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ambapo mrengo wa upinzani pia ulipata mafanikio makubwa. 

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa, wabunge wa upinzani wameibuka na ushindi kwa kupata viti 29 kati ya 50 vya Bunge la nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, ni mwanamke mmoja tu aliyefanikiwa kuingia bungeni naye ni Janan Bushehri, mgombea wa upinzani.

Muundo wa Bunge jipya la Kuwait unafanana sana na lile lililochaguliwa na baadaye kuvunjwa mwaka jana, huku wabunge wote isipokuwa 12 kati ya 50 wakifanikiwa kutetea viti vyao.

Kulingana na Jumuiya ya Uwazi ya Kuwait, shirika lisilo la kiserikali, kiwango cha ushiriki wawananchi katika uchaguzi wa mara hii kilifikia asilimia 50. Hii ni katika hali ambayo, ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wa 63%.

Wakati wabunge nchini Kuwait wanachaguliwa na wananchi kupitia zoezi la kura,  mawaziri wa baraza la mawaziri la nchi hiyo wanateuliwa na familia inayoongoza ya Al-Sabah, ambayo inahodhi nyanja ya kisiasa ya nchi hiyo.

4146341

Kishikizo: kuwait bunge
captcha