IQNA

Khitma ya Qur’ani ya Shahidi Soleimani yafanyika Tehran

21:05 - December 30, 2020
Habari ID: 3473507
TEHRAN (IQNA)- Khitma ya Qur’ani Tukufu imefanyika Tehran Jumanne kwa mnasaba wa kukaribia mwaka moja tokea alipouawa shahidi kamanda wa ngazi za juu wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Khitma hiyo ambayo imewaleta pamoja wasomaji Qur’ani maarufu Wairani imefanyika katika ukumbi wa kidini wa Husseiniya Al Zahra na kuhudhuriwa na viongozi wa kidini na kiutamaduni katika Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO).

Kati ya waliosoma Qur’ani katika kikao hicho ni pamoja na Mohammad Hossein Saeedian, Hadi Movahed Amin, Mehdi Adeli  na Ali Akbar Hanifi.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq Januari 3 mwaka 2020 kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa Iraq.

Punde baada ya kuwasili Iraq aliuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Aidha katika hujuma hiyo ya kigaidi Abu Mahdi Al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq, naye pia aliuawa shahidi akiwa ameandamana na Qassem Soleimani. Watu wengine wanane waliokuwa katika msafara huo nao pia waliuawa shahidi.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na nafasi kubwa katika mapambano na maadui pamoja na magaidi na pia katika kuangamiza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS. Pia alikuwa nguzo muhimu katika harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu katika kusambaratisha njama ya Marekani na Wazayuni ya kuligawa eneo vipande vipande.

3944300

captcha