IQNA

Amir wa Kuwait amtaka waziri mkuu atayarishe uchaguzi

22:27 - October 06, 2020
Habari ID: 3473236
TEHRAN (IQNA)- Amir mpya wa Kuwati amelitaka baraza la mawaziri nchini humo kuendelea na majukumu yake na matayarisho ya uchaguzi mwaka huu baada ya waziri mkuu kujiuzulu.

Waziri Mkuu  Sheikh Swabah al-Khalid al-Swabah alikutana na Amir Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Sabah, ambaye aliapishwa Jumatano. Waziri mkuu amejiuzulu kwa mujibu wa katiba ya nchi ili serikali mpya yenye mani ya amiri mpya ianze kazi.

Taarifa zinasema Sheikh Nawaf ametangaza kuwa na imani na baraza la mawaziri ambalo liliundwa Disemba.

Sheikh Nawaf, 83, alichukua mamlaka baada ya kufa ndugu yake aliyekuwa Amir, Sheikh Swabah, Jumanne iliyopita akiwa na umri wa miaka 91.

Wananchi wa Kuwait sasa wanasubiri kwa hamu kujua ni nani atakayeteuliwa na Sheikh Nawaf kuwa mrithi wa kiti cha ufalme ili amsaidie kuendesha nchi wakati huu bei ya mafuta imeporomoka kufuatia janga la corona na hivyo kuathiri vibaya uchumi wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.  Atakayeteuliwa katika nafasi hiyo anapaswa kuidhinishwa na bunge.
3472747

Kishikizo: kuwait nawaf sabah
captcha