IQNA

Kasisi alaumiwa baada ya benki kufilisika nchini Ghana

16:21 - August 26, 2018
Habari ID: 3471648
TEHRAN (IQNA)-Kasisi wa kanisa moja nchini Ghana amelaumia kusababisha Benki ya Capital nchini humo kuanguka na kuwasabishia wateja hasara kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa Kasisi Mensa Otabil ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Capital aliafiki kutumiwa kinyume cha taratibu GHS milioni 610 ambazo benki hiyo ilizpokea kama msaada kutoka kwa Benki Kuu ya Ghana.

Bada ya kutumia fedha hizo kuinusuru benki hiyo ambayo ilikuwa inaelekea kufilisika, Kasisi Otabil ambaye ni mwanzilishi wa Kanisa la Kimataifa la Central Gospel, aliamuru pesa hizo zitumike kwingine na hivyo kupelekea benki hiyo isambaratike mwaka 2017.

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya benki aliyokuwa akisimamia kufilisika, Kasisi Otabil alisema mara tatu kuwa 'Mungu ni Mzuri" na kudai kuwa hakuwa na kazi za utendaji katika benki hiyo.

Maelfu ya wafanyakazi walipata hasara baada ya benki hiyo kufilisika na hadi sasa hawajaweza kupata pesa zao. Katika kipindi cha miezi ya hivi akribuni benki saba zimefilisika nchini Ghana kutokana na kile ambacho kimetajwa ni usimamizi mbovu.

Hayo yanajiri wakati ambao hivi karibuni wanazuoni wa Kiislamu walitoa wito kwa Benki Kuu ya Ghana kuruhusu mfumo wa Kiislamu wa benki nchini humo ili kuboresha mfumo wa fedha unaokumbwa na msukosuko. Mkurugenzi wa Mabalozi Waislamu Ghana Dr. Abubakar Muhammad Marzuq  amesema mfumo wa Kiislamu wa benki utawanufaisha watu wote wa Ghana bila kujali dini na kuongeza kuwa nchi zingine za Afrika tayari zinafaidika na mfumo wa benki za Kiislamu.

3741288

captcha