IQNA

Senegal yaandaa kongamano la Uislamu na Amani

12:23 - July 30, 2015
Habari ID: 3336950
Kongamano la Kimataifa lenye anuani ya "Uislamu na Amani" limefanyika wiki hii katika mji mkuu wa Senegal, Dhakar.

Kongamano hilo la Jumanne lilihudhuriwa na wasomi, vongozi wa idini, wanaharakati wa kijamii na wanasiasa kutoka nchi kadhaa.
Kongamano hilo lililenga kustawisha amani duniani, kushajiisha ushiriki wa wanawake na vijana katika kuleta amani na kuainisha majukumu ya jamii kuhusu kuimarisha utamaduni wa amani. Halikadhalika mkutano huo ulilenga pia kuondoa dhana potofu kuhusu Uislamu, dini ambayo ni ya amani na rehema. Mkutano huo wa siku moja ulifadhiliwa na Rais Macky Sall wa Senegal.
Senegal ni nchi muhimu katika eneo la Afrika Magharibi ambapo asilimia 92 ya wakazi wake ni Waislamu....mh

3336615

captcha