IQNA

Kongamano la Kimataifa la Tishio la Matakfiri laanza, Qum Iran

11:50 - November 23, 2014
Habari ID: 1476323
Kongamano la Kimataifa kuhusiana na Tishio la Makundi ya Kitakfiri na Yenye Kufurutu Ada limeanza leo katika mji mtukufu wa Qum hapa nchini Iran kwa kuhudhuriwa na masheikh na maulamaa kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kongamano hilo limefunguliwa hii leo na Ayatullahil Udhma Sheikh Nasser Makarem Shirazi mmoja wa maulama na Mar'jaa Taqlidi wakubwa wa nchini hapa  ambaye amesisitiza umuhimu wa Waislamu kuungana, kushirikiana na kupambana na fitna na makundi ya kitakfiri na yenye kufurutu ada.
Ameongeza kuwa, umma wa Kiislamu unapaswa kuwahimiza maulamaa wa Kiislamu watafute suluhisho la matatizo yaliyopo yanayosababishwa na fikra za kitakfiri na kwamba wasitosheke tu na kujadili masuala hayo.
Kongamano hilo la siku mbili linahudhuriwa na maulamaa zaidi ya 300  wa Kishia na Kisuni kutoka nchi 83 duniani huku Iran ikiwakilishwa na Maulamaa 500 wa Kishia na Kisuni…/mh

1476246

captcha