IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Misikiti Nchini Misri Tayari Kukaribisha Mwezi wa Ramadhani

14:27 - March 01, 2024
Habari ID: 3478436
IQNA – Misikiti nchini Misri inatayarishwa kuwakaribisha waumini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wizara ya Wakfu ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika imezindua mpango mkubwa unaojumuisha ukarabati na usafishaji wa misikiti kabla ya mwezi mtukufu.

Mpango huo unatekelezwa kwa kauli mbiu ya “Kutumikia Nyumba za Mungu” na itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa Shaaban, El-Balad News iliripoti.

Mpango huo ni pamoja na kupamba misikiti kwa taa, ambayo imekuwa ni utamaduni wa muda mrefu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani  nchini humo.

Wizara hiyo pia imepanga programu mbalimbali ikiwemo za Qur'ani Tukufu katika msikiti wakati wa Ramadhani.

Programu hizo zinajumuisha vikao vya usomaji wa Qur'ani Tukufu, kozi za Qur'ani Tukufu kuhusu Tajweed na qiraa, na mawaidha.

Mwezi wa Ramadhani, ambao mwaka huu huenda ukaanza Machi 11 mwaka huu kwa kutegemea mwezi mwandamo, ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu.

NI mwezi wa Saumu na kukithirisha ibada  pamoja na kutoa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume (SAW) katika mwezi huu.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji) kuanzia Alfajiri hadi Magharibi.

Waislamu pia wanatumia muda mwingi katika mwezi huu kusoma Qur'ani Tukufu na kutafakari kuhusu aya zake.

4202577

captcha