IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Al-Azhar yawataka Waislamu wasusie bidhaa za Uswidi, Denmark

19:38 - July 26, 2023
Habari ID: 3477345
CAIRO (IQNA) - Kufuatia matukio ya mara kwa mara ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na Denmark, Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimetoa wito kwa Waislamu na nchi za Kiislamu kususia bidhaa za nchi hizo mbili za Ulaya.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano, Al-Azhar iliwataka wananchi wa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuunga mkono Uislamu na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa kugomea bidhaa kutoka Uswidi na Denmark.

Mataifa ya Kiislamu pia yanapaswa kushinikiza serikali zao na mashirika ya Kiislamu kuchukua misimamo ya umoja na ya busara dhidi ya hatua hizo za kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu.

Taarifa hiyo imeeleza kushangazwa na ukimya wa jumuiya ya kimataifa kuhusu jinai hizo ambazo ni sawa na uadui wa moja kwa moja dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Ilitoa wito wa kuharamishwa kuvunjia heshima na kunajisi matakatifu ya kidini katika ngazi ya kimataifa.

Al-Azhar aliendelea kusema kuwa Qur'ani Tukufu ambayo ni kitabu cha mwongozo kwa wanadamu haitadhurika na vitendo hivyo vya kufuru na itabaki kuwa takatifu licha ya majaribio yote hayo.

Katika wiki za hivi karibuni, matukio ya kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Uswidi na Denmark, yanayotokea kwa uungaji mkono wa serikali za nchi hizo mbili, yameibua hasira na kulaaniwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Katika kitendo cha hivi punde zaidi cha kufuru hiyo barani Ulaya, - watu wanaouchukua Uislamu walichoma moto nakala ya Quran mbele ya balozi za Misri na Uturuki mjini Copenhagen siku ya Jumanne.

Kumekuwa na maandamano makubwa katika nchi za Kiislamu kama vile Iran, Iraq, Pakistan, Bangladesh na Yemen kupinga matusi dhidi ya matukufu ya Kiislamu barani Ulaya.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei alisema Jumamosi kwamba watu wanaoivunjia heshima Qur'ani Tukufu wanapaswa kukabiliwa na adhabu kali zaidi.

 

4158150

Habari zinazohusiana
captcha