IQNA

Qarii (msomaji) Qur'ani Tukufu

Abdel Alim Fasada; Qari wa Misri aliyesafiri nchi nyingi kusoma Qur'ani Tukufu

15:18 - January 18, 2023
Habari ID: 3476422
TEHRAN (IQNA) - Sheikh Abdel Alim Fasada alikuwa miongoni mwa wasomaji wakubwa wa Qur'ani Tukufu nchini Misri na alifariki Januari 16, 2021 baada ya miaka mingi ya kujitahidi katika njia ya Qur'ani Tukufu.

Alizaliwa mwaka 1947 katika mji wa Bila katika Jimbo la Kafr El-Shaikh, ambapo alihifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka kumi.

Kisha akasoma sheria za Tajweed na qiraa ya Qur'ani Tukufu chini ya usimamizi wa Sheikh Yusuf Shata.

Baadaye, Fasada alianza kufundisha sayansi za Qur'ani huko Al-Azhar huku pia akihudumu kama qari maalum ya Msikiti wa Al-Ma’adawi katika mji wake wa asili.

Kwa mujibu wa mwanawe, Fasada alisafiri katika nchi nyingi kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, zikiwemo Brazil, Uhispania, Ujerumani na nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu, na alijulikana kuwa balozi bora wa Qur'ani wa Misri.

Alikuwa marafiki na maqari wengine wengi mashuhuri kama vile Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash, Sheikh Mohammed Abdul Wahab al-Tantawi, na Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina.

Mnamo 1999, yeye na qari mwingine Sheikh Mahmoud Sidiq Minshawi walisafiri kwenda Palestina na wote wawili walikuwa wakisoma Qur'ani Tukufu kwenye Msikiti wa Al-Aqsa wakati wa usiku wa Ramadhani.

Mtoto wa Fasada anasema baba yake alikuwa anaanza siku yake kila siku kwa Sala na kisha quraa ya Qur'ani Tukufu.

Anasema mara kwa mara alikuwa akihitimisha Qur'ani (kusoma Quran kuanzia mwanzo hadi mwisho) na alisoma Kitabu kitukufu hadi siku ya mwisho ya maisha yake.

Aliongeza kuwa baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na licha ya ushauri wa madaktari kwamba aache kusoma Qur'ani, alitamani kufa wakati akisoma Kitabu hicho Kitukufu.

Akizungumzia kuhusu Sheikh Fasada, Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina anasema kwamba alikuwa na ujuzi kamili wa kusoma Qur'ani na alikuwa na sauti nzuri pia.

 

4114968

captcha