IQNA

Uislamu Bangladesh

Waziri Mkuu wa Bangladeshi: Uislamu ni dini ya amani, udugu, urafiki

20:10 - January 17, 2023
Habari ID: 3476416
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina aliuelezea Uislamu kuwa ni dini ya amani, udugu na urafiki.

Alisema wananchi wa Bangladesh watapata ujuzi wa kweli wa maadili na utamaduni wa Kiislamu kutoka kwa 'misikiti ya kuigwa' ambayo inafunguliwa nchini humo na halikadhalika katika vituo vya kitamaduni vya Kiislamu ambavyo vitawasaidia kutopotoshwa kwa jina la dini.

Alisema, "Tumechukua miradi ya ujenzi wa 'misikiti ya kuigwa' kwani haiwezi kuwapotosha watu kwa jina la Uislamu na pia itakuwa ikitoa ufahamu juu ya maadili ya Kiislamu."

Waziri Mkuu alisema hayo alipokuwa akifungua misikiti 50 zaidi 'ya kuigwa' nchini kote kwa njia ya video akiwa katika makazi yake rasmi ya Ganabhan Jumatatu (Januari 16).

Waziri Mkuu huyo aliutaja Uislamu kuwa ni dini ya amani, udugu na urafiki na kusema kuwa misikiti hiyo ya mfano itaongeza maarifa ya watu kuhusu Uislamu.

Aliongeza kuwa misikiti hiyo itasaidia pia kukomesha ugaidi, wanamgambo na mateso kwa wanawake kupitia kuwapa watu maarifa ya kweli ya maadili na tamaduni za Kiislamu

Akiwataja wanazuoni kama "Warasatul Anbiya", alisema watu wa nchi hiyo watawaheshimu Khatib (wahubiri) na Maimamu wa misikiti, na kuongeza: "Hakikisha hakuna mtu anayeweza kuwapotosha watu kwa kutumia dini yetu."

"Unaweza kuwafahamisha watu wa kujiepusha kujihusisha na makosa ikiwa ni pamoja na uraibu wa dawa za kulevya, ndoa za utotoni, ukandamizaji dhidi ya wanawake, uzinzi wa chakula na rushwa kwa mahubiri yako ya kila siku na khutba ya Jummah," alisema.

Waziri Mkuu pia alitoa wito kwa wafadhili kusaidia kueneza maadili sahihi ya kibinadamu kati ya watu na kuwasaidia kujiepusha na ugaidi, wanamgambo na uraibu wa dawa za kulevya kwani hizi zinaharibu familia na jamii pia.

3482098

captcha