IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Kizayuni wanatekeleza mauaj makubwa dhidi ya Wapalestina

17:24 - October 22, 2022
Habari ID: 3475973
TEHRAN (IQNA)- NMratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo Yanayokaliwa kwa Mabavu ametangaza katika ripoti yake kwamba mwaka huu wa 2022 ulikuwa mwaka wa umwagaji damu zaidi katika ardhi za Palestina katika kipindi cha miaka 16 iliyopita.

Lucia Elmi amesema mwaka huu wa 2022, Wapalestina wasiopungua 105 wakiwemo watoto 26 wameuawa shahidi na majeshi ya Israel, hivyo mwaka 2022 umekuwa mwaka wa umwagaji damu zaidi tangu 2006. Elmi ameongeza kuwa wastani wa wahanga wa Kipalestina kwa mwezi umeongezeka kwa asilimia 57 ikilinganishwa na mwaka jana.

Swali muhimu ni kwamba, kwa nini ukatili na mauaji ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina mwaka huu wa 2022 yalikuwa ya kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha miaka 16 iliyopita?

Sababu ya kwanza katika suala hili inaweza kuwa inahusiana na aina ya uhusiano kati ya nchi za Kiarabu na utawala ghasibu wa Israel. Katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala unaoikalia kwa mabavu Quds tukufu umeingia katika awamu mpya. Nchi hizo ambazo hapo awali zilikuwa na uhusiano wa siri na utawala wa Kizayuni, katika miaka ya karibuni zimeanzisha uhusiano wa wazi na mpana zaidi na utawala huo haramu. Imarati, Bahrain na Morocco ni nchi tatu za Kiarabu zilizoanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni mwaka 2020 na zimepanua uhusiano huo katika nyuga mbalimbali katika miaka miwili iliyopita. Vilevile nchi kama Saudi Arabia ambazo hazijaanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Israel, pia zimeongeza kiwango cha mahusiano ya siri na utawala wa Kizayuni. Kwa mfano tu, kumefanyika mikutano ya siri kati ya viongozi wa Tel Aviv na Riyadh ndani ya Saudi Arabia, na Riyadh imetoa ruhusa kwa ndege za Israel kuruka juu ya anga ya Saudia. Mabadiliko ya uhusiano kati ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni, kwa upande mmoja, yamekuwa sababu ya nchi hizo kufumbia macho jinai zinazofanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya watu wa Palestina, na kwa upande mwingine Tel Aviv imeendeleza na kuzidisha ukatili dhidi ya Wapalestina kwa damu baridi utulivu mkubwa kwa kutegemea hali hiyo iliyojitokeza katika uhusiano wake na nchi hizo za Kiarabu. 

Sababu ya pili inahusiana na operesheni za muqawama na wanamapambano wa Wapalestina dhidi ya Wazayuni. Wapalestina ambao wamekata tamaa na kupoteza matumaini ya kupata uungaji mkono wa nchi za Kiarabu kwa mapambano yao ya ukombozi dhidi ya utawala wa haramu wa Israel, wamefikia hitimisho kwamba, mapambano na kujitegemea ndio njia pekee ya kukabiliana na jinai za utawala huo ghasibu. Kwa sababu hiyo, mwaka jana operesheni za muqawama dhidi ya Wazayuni zilipanuka zaidi hadi ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, na makumi ya Wazayuni wameangamizwa au na kujeruhiwa katika operesheni hizo. Utawala wa Kizayuni ambao haukuwa na uwezo wa kukabiliana na operesheni hizo, umeamua kutumia mabavu na ukatili zaidi dhidi ya watu wa Palestina.

Sababu ya tatu inahusiana na utendaji wa Umoja wa Mataifa na madola yenye nguvu duniani kuhusiana na kadhia ya Palestina. Ijapokuwa Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo Yanayokaliwa kwa Mabavu amekiri kwamba mwaka 2022 umekuwa mwaka wa umwagaji damu zaidi kwa Wapalestina, umoja huo haukuchukua hatua yoyote ya kulaani jinai za utawala huo ghasibu na kuwaunga mkono Wapalestina. Kwa msingi huo, kama ambavyo siasa za nchi za Kiarabu mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni sababu muhimu ya kuzidishwa jinai za utawala huo ghasibu huko Palestina, kutochukua hatua sambamba na uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa na madola ya Magharibi hususan Marekani kwa utawala huo pia vina athari na mchango katika kushadidi ukatili na mauaji ya Israel dhidi ya watu Palestina.

3480946

captcha