IQNA

Wiki ya Umoja wa Kiislamu

Kongamano la umoja wa Kiislamu ni ishara ya namna Iran inavyozingatia masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu

17:27 - October 12, 2022
Habari ID: 3475918
TEHRAN (IQNA)-Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Iraq amesema, kuandaliwa kongamano la umoja wa Kiislamu kunaonyesha umakini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya ulimwengu wa Kiislamu.

Sheikh Khaled al-Mulla aliyasema hayo Jumatano katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la 36 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu hapa mjini Tehran.

Alianza hotuba yake kwa kutoa pongezi kwa kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Kikosi cha Quds Luteni Jenerali Qassem Soleimani na naibu kamanda wa Vitengo vya Uhamasishaji Maarufu vya Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, ambao waliuawa shahidi katika shambulio la Marekani mnamo Januari 2020.

Amesema Iran inalipa umuhimu suala la Umma wa Kiislamu ikiwemo hali ya Palestina, Lebanon, Iraq na kwingineko, na ndio maana Jamhuri ya Kiislamu ndiyo inayolengwa na chuki.

Al-Mulla ameashiria mivutano ya hivi karibuni na maandamano ya mitaani katika baadhi ya nchi za Kiislamu na kusema kuwa, maadui wameshindwa katika njama zao dhidi ya Umma wa Kiislamu na majaribio ya kuzusha hitilafu kati ya Waislamu wa Shia na Sunni na hivi sasa wanapanga njama za kuzusha ghasia.

Kiburi cha dunia kinalenga kuzusha mizozo na kutaka kupora mali ya Waislamu, alisema na kuongeza kuwa mipango hiyo haitafika popote kwani Umma wa Kiislamu utabaki kuwa na umoja na imara.

Vile vile amepongeza kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW na kusema watu waliabudu masanamu na kueneza ufisadi kabla ya utume wa mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu, kupitia Mtume Wake wa mwisho, alituma mwongozo kwa watu, al-Mulla aliendelea kusema.

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu imeaandaa toleo la 36 la Kongamano la Umoja wa Kiislamu ambapo ushiriki kupitia vikao vya itaneti au webinar ulianza umeanza Oktoba 9 huku kongamano hilo likiwa limefunguliwa rasmi 12 Oktoba na kuendelea hadi Ijumaa. Kongamano la mwaka huu limewashirikisha  wanazuoni wengi wa Kiislamu kutoka nchi 60.

Jumuiya hiyo imekuwa ikiandaa kongamano la kimataifa la Umoja wa Kiislamu kila mwaka kwa muda wa miaka 35 sasa.

Kongamano hilo kwa kawaida hufanyika Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Tuko katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW, siku ambazo ni maarufu kama siku za Maulidi. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal.

Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu. Kwa msingi huo Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu hufanyika katika wiki hiyo ya umoja.

3480825

captcha