Apu hii ya simu za mkononi inamuwezesha mtumiaji kuwa na Qur’ani Tukufu na tafsiri yake na vitabu vingine vya kidini kama vile Mafatihul Jinan popote alipo.
Katika miaka ya hivi karibuni, programu au apu nyingi zimeundwa katika uwanja huu, lakini moja ya programu iliyoundwa vizuri katika kategoria ya kidini inaitwa "habloliman".
Hii ni apu ambayo imekuandalia kozi 48 kwa sauti ya wasomaji mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maeneo mengine ya ulimwengu.
Kama unavyojua, usomaji sahihi wa Qur'ani una umuhimu mkubwa katika Uislamu. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa elimu, watu wengi kwa kawaida hukabiliwa na matatizo katika kusoma Qur’ani kwa usahihi. Lakini apu hii imetatua kabisa tatizo hili kwako.
Moja ya mambo ya kuvutia kuhusu apu hii ni sehemu zake za elimu. Pamoja na kukariri mistari, maana pia ni sehemu muhimu za programu hii. Katika apu huu, maana za aya zote pia zimewekwa kwa watumiaji ili waweze kufahamu na kutafakari kuhusu aya za Qur’ani Tukufu.
Lakini kuzingatia maana pamoja na manufaa yake makubwa inaweza kuwa vigumu kwa watu wakati fulani, hivyo kurejelea tafsiri ni muhimu. Apu hii imekusanya tafsiri bora na za kuaminika za ulimwengu wa Kiislamu, kama vile Al-Mizan, Majam al-Bayan, nk kwa watumiaji wake.
Unaweza kuipakua apu ya habloliman hapa
4089143