Mume na mke walitiwa mbaroni na polisi ya Uturuki baada ya kupatikana wakipiga picha Ikulu ya Rais mjini Istanbul kinyume cha sheria.
Suleima Soylu amesema picha walizopiga jengo hilo hazikuwa zile za kawaida za kitalii bali zilionekana kuwa na ustadi wa juu kwa ajili ya kazi za kijasusi.
Amesema mwendesha mashtaka anaamini kuwa raia hao wa Israel walikuwa wanatekeleza ujasisi na sasa kesi yao itafikishwa mahakamani.
Soylu ni afisa kwa kwanza wa Uturuki kutoa taarifa rasmi baada ya kukamatwa Waisraeli hao wawili Jumatatu. Uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa walipiga picha hizo wakiwa katika mghahawa ulio katika eneo la juu la Mnara wa Mawasiliano wa Camlica Tower ambapo walizituma Israel kupitia WhatsApp huku wakiweka maelezo ya kitaalamu ya picha hizo.
Aidha walituma maelezo kuhusu idadi ya walinzi na taarifa zingine za siru za Mnara wa Mawasiliano wa Camlica, ambao ni mnara mrefu zaidi wa mawasiliano bara Ulaya.