IQNA

Umoja wa Mataifa wapitisha maazimio kadhaa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

19:27 - November 10, 2021
Habari ID: 3474537
TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumanne ilipasisha maazimio sita dhidi ya utawala haramu wa Israel licha ya upinzani mkali wa wawakilishi wa Marekani, Canada na Israel.

Maazimio hayo ya Baraza Kuu la UN yamelaani ukiukaji wa kimfumo wa haki za binadamu za watu wa Palestina, utumiaji mabavu wa Israel dhidi ya raia wa Kipalestina hususan wakazi wa Ukanda wa Gaza na vilevile ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahidi katika ardhi iliyoghusibiwa ya Palestina ikiwemo Quds Mashariki (Jerusalem) na pia Miinuko ya Golan huko Syria. 

Maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pia yametilia mkazo haki ya wakimbizi wa Kipalestina ya kurejea katika ardhi na makazi yao. 

Azimio linalohusiana na eneo la Golan linalokaliwa kwa mabavu pia lieutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza maazimio yaliyopasishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu eneo hilo na kuondoka karika ardhi hiyo ya Syria. 

Itakumbukwa kuwa mwaka 1967 utawala haramu wa Israel ulivamia na kukalia kwa mabavu eneo lenye ukubwa wa karibu kilomita mraba 1,200 la Syria katika Miinuko ya Golan. 

Akihutubia kikao cha Umoja wa Mataifa hiyo jana, mwambata wa ofisi ya mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amlisema, kupitia maazimio sita yaliyopasishwa na Baraza Kuu, kwa mara nyingine tena jamii ya kimataifa imetangaza uungaji mkono wake kwa watu wa Palestina na haki yao ya kujiainishia mambo yao wenyewe. Dr. Mohammad Reza Sahraei pia amesema maazimio hayo yametoa wito wa kuwajibishwa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya raia wa Pelestina wakiwemo wanawake na watoto wadogo.   

4012101

captcha